Alhamisi, 16 Novemba 2017
Siku sahihi ya kuabudu ni ipi
Swali: "Ni siku gani ya sabato, Jumamosi au Jumapili? Wakristo wastahili
kuitunza hii siku?" Jibu: Kila mara husemwa kuwa “Mungu ndiye
alianzisha sabato katika shamba la Edeni” kwa sababu ya uhusiano kati ya
Sabato na uumbaji katika Kutoka 20:11. ingawa starehe ya Mungu siku ya
Sabato (Mwanzo 2:3) iliangazia sheria ya Sabato iliyokua inakuja, hakuna
maelezo yoyote ya Bibilia juu ya Sabato kwa watoto wa Israeli kabla
watoke Misri. Hakuna maandiko katika Bibilia au dondoo lolote
linaloonyesha kuwa Adamu na Musa waliitunza Sabato. Neno la Mungu
laiweka wazi kuwa kuitunza Sabato ilikua ishara maalumu kati ya Mungu na
Waisraeli: “Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli watishika sabato,
kuiangalia sana hiyo sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la
milele. Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku
sita BWANA alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na
kupumzika” (Kutoka 31: 16-16). Katika Kumbukumbu La Torati 5, Musa
anazirudia amri kumi kwa kizazi kingine cha Israeli. Hapa baada ya
kuamrisha jinsi ya kuitunza sabato katika aya ya 12-14, Musa anatoa
sababu ya sabato ambayo sabato ilipewa kwa taifa la Israeli: “Nawe
utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na akuwa
BWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono
ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA Mungu wako, alikuamuru uishike
sabato” (Kumbukumbu La Torati 5:15). Lengo la Mungu kupeana sabato kwa
Waisraeli haikuwa kukumbuka uumbaji, bali waukumbuke utumwa wa Wamisri
na kule kuokolewa na Bwana. Kumbuka yanayohitajika kwa kuitunza sabato:
mtu aliyewekwa chini ya hiyo sheria hangeweza kutoka kwa boma yake
(Kutoka 16:29), hangewakisha moto (Kutoka 35:3), angeruhusu mtu yeyote
kufanya kazi (Kumbukumbu La Torati 5:14). Mtu mwenye angivunja shreria
ya sabato angeuwawa (Kutoka 31:15; Hesabu 15:32-35). Uchunganusi wa
ukurasa wa Agano Jipya watuonyesha mambo mane muimu: 1) Popote Kristo
alionekena baada ya kufufuka kwake na siku zimetajwa, kila wakati ni
siku ya kwanza ya Juma (Mathayo 28:1,9, 10; Mariko 16:9; Luka
24:1,13,15; Yohana 20:19, 26). 2) Wakati pekee sabato imetajwa kutoka
kwa kitabu cha Matendo ya Mitume hadi ufunuo ni kwa sababu ya lengo la
uinjilisti kwa Wayahudi kwenye Masinagogi (Matendo Ya Mitume 13-18).
Paulo aliandika, “Nilikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate
Wayahudi” (1 Wakorintho 9:20). Paulo hakuenda kaitka Masinagogi kuwa na
ushirika na kuwajenga waumini, bali alienda ili awathibitishie injili na
kuwaokoa walikuwa wamepotea. 3) Mara moja Paulo anasema, “tangu sasa
nitakwenda kwa watu wa Mataifa” (Matendo Ya Mitume 18:6), sabato tena
haitajwi kamwe. Na 4) Badala ya kupendekeza kuwa waitunze siku ya
sabato, sehemu nyingine ya Agano Jipya iliyobaki yasema kinyume (
ikijumulisha sehemu ya tatu ilioachwa nche hapo juu, inapatika katika
Wakolosai 2:16). Kwa kuingalia hoja ya nne kwa makini, tutafumbua
kwamba, hakuna jukumu lolote la kuitunza sabato kwa waumini wa Agano
Jipya. Pia tutaonyesha kuwa dhana ya Jumapili “Sabato ya Wakristo” si ya
kibibilia. Vile imejadiliwa hapo juu, hakuna wakati sabato imetajwa
baada ya Paulo kuanza kuangazia Mataifa, “Basi mtu asiwahukumu ninyi
katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa
mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni
wa Kristo” (Wakolosai 2:16-17). Sabato ya Kiyahudi ilifutiliwa msalabani
hamali ambapo Kristo “Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya
kutushitaki” (Wakolosai 2:14). Wazo hili limerudiwa zaidi ya mara moja
katika Agano Jipya: “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku;
mwinginie aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika
akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku huiadhimisha kwa Bwana”
(Warumi 14:5-6a). “Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana
na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge,
yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika siku, na
miezi, na nyaktati, na miaka” (Wagalatia 4:9-10). Bali wengine wanadai
kuwa agizo la Constantino katika mwaka wa 321 A.D (Baada ya Yesu
kuzaliwa) ilibadilisha sabato kutoka Jumamosi hadi Jumapili. Ni siku
gani kanisa la kwanza lilikutana kwa ibada? Bibilia haitaji mkusanyiko
wowote wa sabato (Jumamosi) kwa waumini kwa minajili ya ushirika au
ibada. Ingawa, kuna kurasa wazi zinazoitaja siku ya kwanza ya juma. Kwa
mfano Matendo Ya Mitume 20:7 ambayo yasema, “Hata siku ya kwanza ya
juma, tulipokutana ili kumega mkate.” Katika 1 Wakorintho 16:2 Paulo
anawasihi Wakristo wa Korintho, “Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu
na aweke akiba kwake, kwa kadri ya kufanikiwa kwake.” Jinsi Paulo
anayataja haya matoleo kuwa “huduma” katika 2 Wakorintho 9:12, haya
matoleo lazima yamehuzishwa na ibada ya siku ya Jumapili ya Wakristo.
Kiistoria siku ya Jumapili, bali si Jumamosi ilikuwa siku iliyokubalika
kwa Wakristo katika kanisa na matukio yao yaweza kufuatwa hadi wakati wa
kanisa la kwanza. Sabato ilipeanwa kwa Waisraeli, si kanisa. Sabato
bado ingali siku ya Jumamosi si Jumapili na haijawai badilishwa. Bali
sabato ni sehemu ya sheria ya Agano La Kale na Wakristo wako huru kutoka
kwa mkono wa sheria (Wagalatia 4:1-26; Warumi 6:14). Wakristo
hawitakiwi kuitunza sabato hata kama iko siku ya Jumamosi au Jumapili.
Siku ya kwanza ya juma, siku ya Bwana (Ufunuo 1:10) za sherekea kiumbe
kipya Kristo aliyefufuka akiwa kiongozi wetu. Hatujaamrishwa kiufuata
sheria ya Musa ya sabato ya kustarehe, bali tuko huru kumfuata Kristo
aliyefufuka. Mtume Paulo alisema kwamba kila mkristo amue mweneyewe kama
ataifuata sabato, “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku;
mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika
akili zake mwenyewe” (Warumi 14:5). Twastahili kumwabudu Mungu kila
siku, si Jumamosi pekee or Jumapili pekee.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
MAKUNDI MAWILI YA WATU WANAOKUZUNGUKA.
FAHAMU MAKUNDI MAWILI YA WATU KATIKA MAISHA YAKO. Na Steven Mshiu . Maisha ya kila mwanadamu yamezungukwa na watu. Watu hawa waweza kat...
-
KUNA HAJA YA KANISA KUOMBA KWA AJILI YA VIJANA Na Steven Mshiu. Siku mbili zilizopita nikiwa katika tafakari yangu binafsi juu ya musta...
-
UNAJUA MAHALI SAHIHI PA KUWEKA TUMAINI LAKO? Na Steven Mshiu, Habari mpenzi msomaji wa makala zangu. Ni matumaini yangu u bukhe...
-
NGUVU YA USHUHUDA. Na Steven Mshiu. Habari za leo mpendwa rafiki. Naamini una uzima wa kutosha kabisa. Ni jambo la kumshukuru Mungu san...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni