Jumanne, 17 Oktoba 2017

WEKA TUMAINI LAKO KWA MUNGU.



UNAJUA MAHALI SAHIHI PA KUWEKA TUMAINI LAKO?

Na Steven Mshiu,
Habari mpenzi msomaji wa makala zangu. Ni matumaini yangu u bukheri wa afya, na unaendelea kujifunza mengi kupitia blog yetu hii ambayo kila siku inazidi kuwa na watembeleaji wengi. Hili linanitia moyo maana ninatambua kuwa kazi ninayoifanya sio bure.

 Tumelenga kuwafikia watu wote kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuelimishana kama tunavyofanya hapa, kwa njia mbalimbali na huduma nyinginezo zinazomgusa Mungu wetu. Karibu uungane nasi.

Leo katika mfululizo wa makala zangu napenda kukushirikisha kuhusu "TUMAINI". Nianze kwa kusema hivi, Biblia inasema katika Zaburi 125:1 "Wamtumainio Bwana ni kama mlima sayuni ambao hautatikisika nao wakaa milele."

Je wewe umeweka tumaini lako wapi? Unajua tunaishi katika nyakati ambazo hatuoni tena utendaji wa Mungu katika maisha yetu, maana tumaini na tegemeo letu halipo tena kwake. Tumekuwa ni watu wa kutegemea akili zetu wenyewe. Hatujali tena chanzo cha maarifa yetu. Mahali fulani Biblia ikasema, Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, nae aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa. Kumbe akili zetu pasipo ni bure kabisa. Warumi 1:28

Hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia mauaji ya kinyama kabisa kwa albino na mambo ya ajabu ajabu tu. Kwanini? Wale wanofanya hivyo si kwamba hawajui, lakini kwa sababu kuna mganga amemwambia afanye hivyo basi tumaini lake ameliweka kwa huyo mganga. Fikiria ni kiongozi wa nchi halafu tumaini lake ni kwa waganga na wachawi, halafu anataka aongoze nchi. Inawezekana? Mungu hawezi kukupa nafasi hiyo hata siku moja maana ameshakuacha ufuate akili yako isiyofaa.

Ndugu mpendwa, mahali sahihi pa kuweka tumaini lako ni kwa mungu tu. Soma mithali 16:3 mkabidhi mungu njia zako na mawazo yako yatathibitika. Haijalishi umemaliza chuo miaka minne imepita bado hujapata ajira, mtumaini mungu,. Umeanzisha biashara, haiendi vizuri. Usiende kwa mganga. Kila unalolifanya haliendi, mtumaini MUNGU tu.

Nikutie moyo, bado hujachelewa. Una nafasi ya kufanya mambo makubwa tena makubwa sana. Tambua
kuwa mafanikio yako yanategemea ni wapi ulipoweka tumaini lako. Ilipo hazina ya mtu ndipo na moyo wake ulipo. Mafanikio yanayopatikana kirahisi(kwa waganga) hayadumu. Yale yanayotoka kwa MUNGU huwa ni ya baraka sana.. Jifunze kwa "super nation" Marekani,. Kwenye dolla yao utaona rais amenyoosha mkono juu halafu kuna maandishi haya, "IN GOD WE TRUST"

Ndio maana taifa hilo kubwa duniani linaendelea kubaki katika ubora wake, mataifa mengi yanalitegemea kwa njia moja au nyingine. Thamani ya pesa yao iko juu. Kwanini? Wametambua kuwa tumaini na tegemeo lao linastahili kuwa kwa MUNGU.

Nimalizie hivi kwa leo. Unapomtegemea au kuweka tumaini lako kwa mtu au kitu mfano wachawi, waganga, ushirikina n.k, hauna tofauti na kutegemea jino lililovunjika, siku ukiletewa nyama yenye mifupa utabaki unaikodolea macho tu.

Weka tumaini lako kwa MUNGU wako rafiki.
Ahsante na ubarikiwe sana.
Kumbuka: "OUR SUCCESS IS YOURS"

Mwandishi: Steven I. Mshiu
0655882074
smshiu42@gmail.com.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MAKUNDI MAWILI YA WATU WANAOKUZUNGUKA.

FAHAMU MAKUNDI MAWILI YA WATU KATIKA MAISHA YAKO. Na Steven Mshiu . Maisha ya kila mwanadamu yamezungukwa na watu. Watu hawa waweza kat...