Jumanne, 17 Oktoba 2017

UJIONAVYO NDIVYO UTAKAVYOKUWA



UJIONAVYO NDIVYO UTAKAVYOKUWA..

Na Steven Mshiu,
Habari mpenzi msomaji wa makala zangu. Ni matumaini yangu kuwa u bukheri wa afya na muendelezo mzuri katika kujenga taifa ambalo bado kwa njia moja au nyingine linaonekana kutoimarika. Nikutie moyo kuwa kazi yako ni njema na ina thawabu kwani huwezi kulima shamba leo na uvune leo leo.

Leo katika mfululizo wa makala zangu ninakuletea makala hii, "UJIONAVYO NDIVYO UTAKAVYOKUWA" Kama unavyojua kuwa kabla mtu hajafanya jambo/kitu fulani huwa kuna hali inayoanza kujijenga ndani yake, yaweza kuwa kushindwa au kushinda, kujidharau, au kijiona jasiri n.k.

Kumbuka hakuna mwanadamu alieumbiwa kushindwa, kujidharau, au kukata tamaa, sema ni zile changamoto tunazokutana nazo zinatupelekea kuingia katika hali hiyo. Hivyo ni lazima ukabiliane nayo na usikubali ikushinde.

Tukisoma katika Biblia tunaona kuwa ilifika mahali katika safari ya wana wa Israel kwenda Kanaani, wamekaribia kabisa MUNGU anamwambia Musa atume watu 12 wakaipeleleze nchi ya Kanaani, miongoni mwao yupo JOSHUA na KALEBU.

Na walipofika kuipeleleza nchi ya kanaani walikuta ina kila kitu, maziwa, asali, zabibu nk, hivyo walikuwa na kila sababu ya kuimiliki nchi ile.

Lakini tatizo walilokutana nalo ni uimara wa mji ule pamoja na watu wanaokaa katika nchi ile ndio waliowakatisha tamaa na kujidharau kuwa hawawezi kuirithi nchi ile ambayo MUNGU alikuwa amewaahidi.
 

Ona wanavyosema katika Kutoka 13:33 kisha huko tuliwaona Wanefili wana wa Anaki....."tukajiona­ nafsi zetu kama mapanzi" "nao ndivyo walivyotuona sisi"

Lakini Kalebu na Yoshua wanawatia moyo watu kuwa wapande na kuimiliki nchi hiyo, na kwa sababu wameshaathirika kisaikolojia wakajiona kuwa hawawezi kabisa. Matokeo yake wote wanafia pale jangwani, lakini Yoshua na Kalebu wao wanairithi nchi.

Je wewe unajionaje, unaona kushindwa au kukata tamaa? Inuka endelea na mapambano.


Ubarikiwe sana.
Imeandaliwa na
Steven I. Mshiu
0655882074
smshiu42@gmail.com,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MAKUNDI MAWILI YA WATU WANAOKUZUNGUKA.

FAHAMU MAKUNDI MAWILI YA WATU KATIKA MAISHA YAKO. Na Steven Mshiu . Maisha ya kila mwanadamu yamezungukwa na watu. Watu hawa waweza kat...