JIFUNZE KUTOKA KWA NDEGE WA ANGANI.
Na Steven Mshiu
Ndege ni miongoni mwa viumbe hai aliowaumba Mungu. Na alipowaumba aliwaweka chini ya utawala wa mwanadamu. Maisha ya ndege ni ya uhuru sana. Yupo tayari kwenda popote pale anapopataka tena kwa wakati.
Mungu alipowaumba alifafahamu kuwa watakula wapi na watalala wapi. Mahali pengine Yesu mwenyewe akasema tusisumbukie maisha yetu, tuwaangalie ndege wa angani. Wao hawana shamba lakini Mungu huwalisha. Sasa kwetu sisi wanadamu si zaidi ya hao ndege?
Maisha ya ndege hutegemea kiota kama sehemu ya kulala, kuishi na kuzaliana. Kiota hicho mara nyingi ndege hukijenga kwenye tawi linaloningi'inia. Hutumia muda mrefu kukijenga kiota hicho. Tulipokuwa watoto tulikuwa tukiviharibu viota hivyo, lakini cha ajabu ndege yule huangalia tawi lingine na kuanza kujenga kiota kingine kipya.
Kiota kile hukitumia kwa muda hasa pale anapojiandaa kutaga, na baada ya kumaliza kutaga huyaatamia yale mayai hatimaye hutotoa makinda ya ndege.
Hutumia juhudi nyingi kuhakikisha yale makinda yanakuwa ndege kamili, na baada ya hapo huhama kwenye kiota kile na kusonga mbele kwa mbele. Maisha yanaendelea kama kawaida.
Kitu nilichotaka tujifunze kupitia ndege ni kwamba yeye anategemea ule uwezo aliopewa na Mungu, Jana nilikuwa nakatiza maeneo fulani nikakutana na kundi kubwa sana la ndege. Walikuwa wamekusanyika kwenye mti uliokuwa na matawi mengi sana, Kwa kuwa ilikuwa ni majira ya jioni hivyo upepo ulikuwa ukivuma,
Niliyaona matawi yakienda huku na kule, yaani yakienda jinsi upepo ulivyokuwa ukivuma. Lakini jambo la kushangaza sikuwaona wale ndege wakihofia matawi labda kutokana na upepo kuwa mkali, tawi linaweza kuvunjika hivyo likahatarisha maisha yao.
Nilipoendelea kuwaza zaidi ndipo nikakumbuka kuwa ndege hawategemei sana yale matawi ya ule mti. tegemeo kubwa la ndege lipo kwenye mbawa zake. Kama tawi likivunjika wakati wowote, basi wataruka kwa kutumia msaada wa mbawa zao na kutafuta tawi lingine.
MAMBO YA KUJIFUNZA
Kuna watu Mungu amewapa vitu vizuri sana ikiwa ni pamoja na akili lakini hawajui ni kwanini au ni kwa sababu gani wamepewa.
Mara nyingi katika maisha yrtu kuna mambo au changamoto tunakutana nazo zinatufanya tuondoe lengo kwa Mungu na kuliweka sehemu fulani. Unaweza kuwa unasoma mchakato wa ada ukawa ni mgumu ukaweka tumaini lako kwa ndugu yako maana ana uwezo kidogo. Nataka nikukumbushe kuwa huyo ndugu ni kama tawi. Kuna siku upepo utavuma halafu litavunjika. Jiulize kama ndio umeshika kwenye tawi hilo matokeo yake yatakuwaje?
Kuna watu Mungu amewabariki kwa vitu vichache tu. Wakasahau kuwa ni Mungu kawawezesha kuvipata. Imani yao wakaiweka kwenye vitu hivyo. Hawana tena hata muda wa kumfanyia Mungu ibada. Mtu yuko bize jumatatu hadi jumatatu. Nakukumbusha kuwa vitu hivyo ni kama tawi tu. Siku upepo ukivuma kwa kasi yawezekana tawi hilo likavunjika. Upepo naufananisha na majaribu. Mpendwa hali yako itakuwa ni mbaya zaidi.
Kuna watu wana nia ya kufanya mambo makubwa kwa ajili ya kutimiza kusudi Mungu alilowaumbia. Lakini hali ya kukatishwa tamaa na kurudishwa nyuma inapowakabilli basi basi huona ni bora kuishia njiani kabisa. Hukata tamaa na kurudi nyuma. Tulipoharibu viota vya wale ndege, kesho yake tulikuta wamejenga kiota kipya tayari.
Maisha yanahitaji watu jasiri. Watu wasiokata tamaa. Watu wasiochoka kujaribu kufanya kitu kipya. Mungu naye anamhitaji mtu asiyeangalia nyuma. Kuangalia nyuma ni ishara ya kushindwa, Muulize mke wa Lutu kilichomkuta kisa kuangalia nyuma. Askari anaeangalia nyuma au kurud nyuma hupigwa risasi na kikosi kinachobakia husonga mbele kwa ajili ya kuutafuta ushindi.
Jaribu kufanya kitu kipya leo.
Ishi maisha yenye UHURU. Nikisema maisha yenye uhuru simaanishi ufanye unavyotaka. Ndege wana uhuru wa kutosha. Hakuna kiumbe kinachowapigia kengele kuwa muda wa kuamka umefika. Hakuna kiumbe kinachowaambia kuwa ni muda wa kwenda kutafuta chakula, au ni muda wa kurudi kwenye kiota chake. Wao wamejipangia ratiba zao vizuri. Uhuru unatokana na kujijengea nidhamu binafsi.
Kuna watu wanapokuwa karibu na wazazi wao huishi maisha fulani na wanapotoka karibu na wazazi wao huishi maisha tofauti kabisa. Yaani mtu ana wokovu wa nyumbani tu, Akitoka nyumbani hana wokovu. Biblia inasema katika Yohana 8; 33 na kuendelea kuwa mtu anapoifahamu KWELI huwa HURU kwelikweli.
Jifunze kujitegemea. Mungu hakumuumba mtu ili awe tegemezi. Utegemezi huanza pale mtu anapojisahau na kutoka kwenye lengo lake yaani kusudi. Ndege wao hawamtegemei mtu. Tegemeo lao kubwa lipo kwa aliewaumba tu. Pale unapoonyesha juhudi zako kuwa unaweza ndipo Mungu naye hukuwezesha. Epuka kumtegemea mtu au kitu, maana wakat wowote vitu vyaweza toweka. watu nao waweza toweka.
Jambo la mwisho kumbuka kuwa Mungu amekupa uwezo wa kuhimili kila aina ya kimbunga au upepo unaovuma katika maisha yako. Hakuna mwanadamu ambaye anaweza kuyakwepa majaribu. Imani yetu ni kama mbawa za ndege. Pale kimbunga cha majaribu kinapotaka kutuzamisha basi kupitia mbawa za imani yetu tunaweza kuruka juu zaidi na tukafikia ushindi mkubwa sana.
Mpendwa rafiki,
Natamani niendelee kuandika zaidi na zaidi lakini kwa machache haya ni imani yangu kuwa kuna jambo moja au mawili utakuwa umejifunza.
Nakutia moyo kuwa huna sababu hata moja ya kuishia njiani ila una sababu nyingi tu za kuinuka na kusonga mbele na hatimaye ukaweza kufikia USHINDI MKUBWA SANA.
Mungu akubariki sana kama utasoma waraka huu hadi mwisho na ukiupenda waweza mshirikisha na mwenzio.
Rafiki yako.
Steven Mshiu
+255 655 882074
+255 768 882074
smshiu42@gmail.com

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni