
Sikupenda siku ya leo ipite hivi hivi bila kukukumbusha angalau kitu kimoja.
Siku mbili zilizopita nilikuwa nina shida na mtu fulani, na nisingeweza kumpata pasipo kutumia mawasiliano ya simu. Kwa bahati nzuri nina simu ya mkononi. Kilichofuata niliamua kununua vocha yenye thamani ya shs. 5,000/-
Kwa kuwa mtu niliyetaka kuwasiliana naye alikuwa yupo nje nje ya nchi ilinibidi niihifadhi ile vocha kwa umakini mkubwa saaana, niliitunza sana kwa muda wa masaa saba hivi, akili yangu yote ilikuwa ikiiwaza ile vocha. Kwamba muda utafika saa ngapi ili niitumie,
Ilipofika majira ya saa nne na nusu hivi nyakati za usiku tayari giza lilikuwa limeshaifunika dunia, niliitoa ile vocha na kuwasha tochi ya simu yangu hatimaye nikaibadilisha ile vocha kuwa muda wa maongezi.
Baada ya kuiingiza ile vocha kwenye simu yangu kabla sijazima tochi ya simu tayari kile kikadi cha vocha chenye thamani ya 5000 nilishakitupa chini na kukisahau, kwani ile thamani yake ilishahamia kwenye simu yangu.
Cha ajabu sikuwa na muda wa kuiwazia tena ile kadi. HAtimaye nikafanya mawasiliano na yule ndugu niliyekusudia na mambo mengine yakaendelea.
Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Roho Mtakatifu akaanza kunifundisha vitu vyake.
Nikajifunza kuwa maisha yetu yana thamani kubwa sana, ni zaidi ya thamani ya madini ya aina yoyote ile.
Akanifundisha kuwa miili yetu huwa na thamani kabla haijatumika vibaya. Ikishatumika vibaya ule ubora wake hupotea kabisa,
Sasa basi acha leo niwakumbushe vijana wenzangu hususani mabinti. Nimekuwa nikisikia kuwa kuna mabinti ambao wamefanya miili yao kama chanzo cha mafanikio. Kuna ambao wako vyuoni lakini ili wafaulu wanaamua kuitoa miili yao kwa walimu ili wasifeli. Wengine ili wapate kazi wanadiriki kulala na waajiri wao ilhali wapate ajira tu.
Yaani hawaamini kama Mungu anaweza kuwapa kile wanachohitaji pasipo kutoa rushwa ya miili yao.
Leo nataka nikukumbushe jambo hili. Hao unaojirahisisha kwao wamekufanya Kuwa kama VOCHA. Wanakuthamini kabla hawajakutumia. Ile haja ya nafsi zao yenye uovu ikishatimia wanakutupa kama mimi nilivyotupa ile kadi ya VOCHA niliyokwisha kuitumia,
Wakishakutumia watakutupa. Tena watakutupa gizani. Tena wakiwa wamezima taa. Hawatakujali tena. Huyo lecturer akishamaliza haja yake atatafuta mwingine tena. Hata mimi baada ya kuitumia ile vocha ilipokwisha nilienda kutafuta nyingine siku iliyofuata. Huyo kijana unaeenda kujirahisisha kwake, eti ni wachumba unakaa kwake, sijui unamfulia eti kakuambia atakuoa, mwishowe anakuingiza chumbani na kutekeleza azma yake aisee ukishafanya hivyo ndio imekula kwako.
Tayari hapo ni VOCHA imeshatumika mzee, Jiandae kisaikolojia kutupwa na kukanyagwa na watu wengine. Na usitegemee tena ile thamani yako kurudi.
Vijana wenzangu tujiheshimu. Tusikubali mtu yeyote atutumie kama anavyopenda yeye. Tunahitaji kuitunza thamani yetu.
Mara nyingi huwa napenda kusema kauli hii kuwa JIHESHIMU ILI UHESHIMIWE. Hakuna mtu atakayekuheshimu ilhali wewe umeshaji-devaluate.
Ukitaka watu wakusifu ni pale unapoonyesha msimamo wako na uthamani wako.
Leo una nafasi ya kumwonyesha huyo lecturer kuwa wewe ni wa thamani ipi,
Una nafasi ya kumwonyesha huyo Bosi kuwa wewe ni wa thmani ipi.
Una nafasi ya kumwonyesha huyo kijana anayekudanganya kuwa wewe sio wa bei rahisi.
Una nafasi ya kuonyesha uthamani wako.
Zile sifa zitakazotoka kwa watu, kama anavyosifiwa binti aliyeitunza thamani yake katika Mithali 31:29, utazisikia kwa wengine tu. Wale waliokataa kuipoteza thamani yao.
Nikutie moyo ewe binti, Ingawa unakutana na changamoto hizi nyingi, Usijaribu kutumika kama VOCHA. Itunze thamani yako. Jiamini kuwa unaweza bila hata kuutumia mwili wako kama chanzo, cha kupata mafanikio. Mungu amekupa akili na uwezo. Itumie akili na uwezo vyema hakika utafanikiwa.
Ondoa ile dhana kuwa ukiutoa mwili wako bwererer bwerere ndio utapata mafanikio ya haraka kwa kirahisi. Aliwahi nifundisha mtu mmoja kuwa siku zote RAHISI NI GHALI ZAIDI. Kile kitu unachokipata kwa urahisi kwa kutumia njia rahisi rahisi huwa kinagharimu sana.
Nataka leo uchukue hatua. Hatua ya kumwonyesha kila mtu thamani yako.
Baada ya muda mchache utakuja kunipa ushuhuda wa ushindi mkubwa sana wenye matokeo chanya.
Kama ujumbe huu utakugusa natoa ruhusa ya kuu-share popote pale ili tuwakumbushe wengine kuitunza thamani yao.
Ubarikiwe sana.
Rafiki yako,
Steven Mshiu.
+255 655 882074
+255 768 882074,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni