THAMANI YAKO NI ZAIDI YA CHOCHOTE.
Na Steven Mshiu.
Sikupenda siku ya leo ipite hivi hivi bila kukukumbusha angalau kitu kimoja.
Siku mbili zilizopita nilikuwa nina shida na mtu fulani, na nisingeweza
kumpata pasipo kutumia mawasiliano ya simu. Kwa bahati nzuri nina simu
ya mkononi. Kilichofuata niliamua kununua vocha yenye thamani ya shs.
5,000/-
Kwa kuwa mtu niliyetaka kuwasiliana naye alikuwa yupo nje
nje ya nchi ilinibidi niihifadhi ile vocha kwa umakini mkubwa saaana,
niliitunza sana kwa muda wa masaa saba hivi, akili yangu yote ilikuwa
ikiiwaza ile vocha. Kwamba muda utafika saa ngapi ili niitumie,
Ilipofika majira ya saa nne na nusu hivi nyakati za usiku tayari giza
lilikuwa limeshaifunika dunia, niliitoa ile vocha na kuwasha tochi ya
simu yangu hatimaye nikaibadilisha ile vocha kuwa muda wa maongezi.
Baada ya kuiingiza ile vocha kwenye simu yangu kabla sijazima tochi ya
simu tayari kile kikadi cha vocha chenye thamani ya 5000 nilishakitupa
chini na kukisahau, kwani ile thamani yake ilishahamia kwenye simu
yangu.
Cha ajabu sikuwa na muda wa kuiwazia tena ile kadi.
HAtimaye nikafanya mawasiliano na yule ndugu niliyekusudia na mambo
mengine yakaendelea.
Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Roho Mtakatifu akaanza kunifundisha vitu vyake.
Nikajifunza kuwa maisha yetu yana thamani kubwa sana, ni zaidi ya thamani ya madini ya aina yoyote ile.
Akanifundisha kuwa miili yetu huwa na thamani kabla haijatumika vibaya. Ikishatumika vibaya ule ubora wake hupotea kabisa,
Sasa basi acha leo niwakumbushe vijana wenzangu hususani mabinti.
Nimekuwa nikisikia kuwa kuna mabinti ambao wamefanya miili yao kama
chanzo cha mafanikio. Kuna ambao wako vyuoni lakini ili wafaulu wanaamua
kuitoa miili yao kwa walimu ili wasifeli. Wengine ili wapate kazi
wanadiriki kulala na waajiri wao ilhali wapate ajira tu.
Yaani hawaamini kama Mungu anaweza kuwapa kile wanachohitaji pasipo kutoa rushwa ya miili yao.
Leo nataka nikukumbushe jambo hili. Hao unaojirahisisha kwao
wamekufanya Kuwa kama VOCHA. Wanakuthamini kabla hawajakutumia. Ile haja
ya nafsi zao yenye uovu ikishatimia wanakutupa kama mimi nilivyotupa
ile kadi ya VOCHA niliyokwisha kuitumia,
Wakishakutumia
watakutupa. Tena watakutupa gizani. Tena wakiwa wamezima taa.
Hawatakujali tena. Huyo lecturer akishamaliza haja yake atatafuta
mwingine tena. Hata mimi baada ya kuitumia ile vocha ilipokwisha
nilienda kutafuta nyingine siku iliyofuata. Huyo kijana unaeenda
kujirahisisha kwake, eti ni wachumba unakaa kwake, sijui unamfulia eti
kakuambia atakuoa, mwishowe anakuingiza chumbani na kutekeleza azma yake
aisee ukishafanya hivyo ndio imekula kwako.
Tayari hapo ni VOCHA
imeshatumika mzee, Jiandae kisaikolojia kutupwa na kukanyagwa na watu
wengine. Na usitegemee tena ile thamani yako kurudi.
Vijana wenzangu tujiheshimu. Tusikubali mtu yeyote atutumie kama anavyopenda yeye. Tunahitaji kuitunza thamani yetu.
Mara nyingi huwa napenda kusema kauli hii kuwa JIHESHIMU ILI
UHESHIMIWE. Hakuna mtu atakayekuheshimu ilhali wewe umeshaji-devaluate.
Ukitaka watu wakusifu ni pale unapoonyesha msimamo wako na uthamani wako.
Leo una nafasi ya kumwonyesha huyo lecturer kuwa wewe ni wa thamani ipi,
Una nafasi ya kumwonyesha huyo Bosi kuwa wewe ni wa thmani ipi.
Una nafasi ya kumwonyesha huyo kijana anayekudanganya kuwa wewe sio wa bei rahisi.
Una nafasi ya kuonyesha uthamani wako.
Zile sifa zitakazotoka kwa watu, kama anavyosifiwa binti aliyeitunza
thamani yake katika Mithali 31:29, utazisikia kwa wengine tu. Wale
waliokataa kuipoteza thamani yao.
Nikutie moyo ewe binti, Ingawa
unakutana na changamoto hizi nyingi, Usijaribu kutumika kama VOCHA.
Itunze thamani yako. Jiamini kuwa unaweza bila hata kuutumia mwili wako
kama chanzo, cha kupata mafanikio. Mungu amekupa akili na uwezo. Itumie
akili na uwezo vyema hakika utafanikiwa.
Ondoa ile dhana kuwa
ukiutoa mwili wako bwererer bwerere ndio utapata mafanikio ya haraka kwa
kirahisi. Aliwahi nifundisha mtu mmoja kuwa siku zote RAHISI NI GHALI
ZAIDI. Kile kitu unachokipata kwa urahisi kwa kutumia njia rahisi rahisi
huwa kinagharimu sana.
Nataka leo uchukue hatua. Hatua ya kumwonyesha kila mtu thamani yako.
Baada ya muda mchache utakuja kunipa ushuhuda wa ushindi mkubwa sana wenye matokeo chanya.
Kama ujumbe huu utakugusa natoa ruhusa ya kuu-share popote pale ili tuwakumbushe wengine kuitunza thamani yao.
Ubarikiwe sana.
Rafiki yako,
Steven Mshiu.
+255 655 882074
+255 768 882074,
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
MAKUNDI MAWILI YA WATU WANAOKUZUNGUKA.
FAHAMU MAKUNDI MAWILI YA WATU KATIKA MAISHA YAKO. Na Steven Mshiu . Maisha ya kila mwanadamu yamezungukwa na watu. Watu hawa waweza kat...
-
KUNA HAJA YA KANISA KUOMBA KWA AJILI YA VIJANA Na Steven Mshiu. Siku mbili zilizopita nikiwa katika tafakari yangu binafsi juu ya musta...
-
UNAJUA MAHALI SAHIHI PA KUWEKA TUMAINI LAKO? Na Steven Mshiu, Habari mpenzi msomaji wa makala zangu. Ni matumaini yangu u bukhe...
-
NGUVU YA USHUHUDA. Na Steven Mshiu. Habari za leo mpendwa rafiki. Naamini una uzima wa kutosha kabisa. Ni jambo la kumshukuru Mungu san...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni