MAMBO SITA YA MSINGI ANAYOTAKIWA NAYO KIJANA ILI AWEZE KUKUBALIKA KATIKA JAMII.
Na, Steven Mshiu.
Leo ninawiwa kukuletea makala hii, "MAMBO 6 YA MSINGI ANAYOTAKIWA KUWA NAYO KIJANA ILI AKUBALIKE KATIKA JAMII". Lakini acha nianze kwa kusema hivi, binafsi nina hofu kubwa sana kwa "taifa la kesho" ambalo asilimia kubwa ni sisi vijana maana tumekosa muelekeo, na kupoteza uthamani wetu.
Taifa linategemea vijana, familia kama familia inategemea vijana, makampuni mengi yanategemea vijana, hata kanisa nalo linategemea vijana, kwanini? Kwa sababu vijana tuna nguvu, yani ni tofauti na watu wa umri mwingne kama wazee na watoto. Hata biblia inasema hivyo. Lakini cha ajabu tumeshindwa kujitambua kuwa sisi ni akina nani na tunapaswa kufanya nini. Ole wetu vijana.
Kutokana na hali hii jamii imeshindwa kutupa kipaumbele kwa ajili ya kukosa mambo haya sita ambayo tutayaangalia japo kwa kifupi kutoka 1 Thimotheo 4:11-12, Mwandishi wa maneno haya alikuwa ni Paulo aliyejulikana kwa jina la Sauli ambaye alikuwa na kazi ya kuwaua watumishi wa Mungu waliokuwa wakiifundisha KWELI ya MUNGU. Na alikuwa akimwandikia mwanae katika huduma aliyejulikana kwa jina la Timotheo.
Ingawa Timotheo alikuwa ni mdogo kiumri, lakini Paulo alitaka kumthibitishia kuwa atakapotambua kile kilichopo ndani yake yaani kusudi lake hakika jamii itamheshimu na pia itaheshimu ile huduma yake. Mwandishi anasema mtu yeyote asiudharau ujana wako bali uwe.
1. Kielelezo.
Kuwa kielelezo ina maana ni kuwa mfano, kitu cha kuigwa. Watu wa"copy" kutoka kwako. Sasa tumekuwa hatuna cha kuigwa katika jamii, badala yake ndo walevi "wanywa viroba" kuwa na tabia zisizo njema kama wizi, uporaji n.k.
Ukija kwenye suala la uvaaji ndio hatari kabisa, dada zetu wanavaa nguo zinazonesha miili yao"transparency" vijana wa kiume nao suruali chini ya makalio,. Yani jamii inashindwa kutuelewa kabisa. Vijana wengi wa siku za leo hatuna kitu chochote ambacho jamii itaiga kwetu. Hii ni hatari kubwa sana. Hebu tubadilike.
2. Usemi.
Kauli/usemi ndiyo inayomfanya mtu kukubalika mahali popote pale. Watu wanakutambua kwa jinsi unavyoongea tu. Kwa utafiti mdogo nilioufanya nimegundua kuwa vijana ndio wenye majibu ya "hovyo" mahali popote pale. Ukikuta binti anajibizana na mama yake huwezi amini kama anamjibu mzazi wake hvyo.
Sasa kupitia kauli zetu na jinsi tunavyo"communicate"¬ na watu kumetufanya tukawa tunakosa fursa mbalimbali na hata kushirikishwa kwenye jambo lolote lile linalohitaji maamuzi au mchango wa kijana. Hali hii inatufanya tunakosa haki zetu za msingi.
3. Mwenendo
Jamii inatazamia kuwa mwenendo wa kijana unatakiwa kuwa mzuri, lakini badala yake, inatuona tunaenenda katika njia zisizofaa kama ukahaba, ulevi, wizi na kujiunga na vikundi vya uhalifu n,k, jamii inatudharau. Kumbuka nilianza kwa kusema kuwa "mtu yoyote asiudharau ujana wako" lakni hapa sisi tunakuwa chanzo cha kudharaulika. Hebu tubadilishe mwenendo wetu kuwa mzuri.
4. Upendo.
Kama kijana utakosa kuwa na upendo kwa jamii inayokuzunguka, itakuwa ni ngumu sana kupata msaada. Jamii itakutelekeza. Ukitaka jamii yako ikupende, ipende wewe kwanza. Kila mtu atatamani kuuona uwepo wako. Fursa nyingi zitakua zinakuangukia wewe maana una mahusiano mazuri na jamii yako.
5. Imani.
Hili ni jambo lingne la muhimu sana kwa maisha ya kimwili na kiroho. Ili umpendeze Mungu ni lazima kuwa na imani. Biblia inasema kuwa "Hauwezi kumpendeza Mungu kama huna imani". Jamii inapenda mtu anaemwamini Mungu, maana hata yeye mwenyewe ataaminika. Siku hizi ofisi nyingi zinaogopa kuwaajiri vijana, kwa sababu hazina imani na sisi. Tunakosa mambo mengi kwa sababu hatuamiki. Tubadilike. Tukitaka kula "mema ya nchi" hebu tujiaminishe kwa jamii. Tusiwe watu wa kutiliwa mashaka kila mahali.
6. Usafi.
Hapa sizungumzii usafi wa kimwili tu. Maana mwili huu ni kama "mother body" ya roho zetu. Japo ni lazima uuweke katika hali nzuri. Hata biblia inasema itunzeni miili yenu maana ni hekalu la roho mtakatifu. Utakapoamua kuwa msafi kiroho, yaani kuacha mambo yote mabaya i.e dhambi, hata kimwili utakuwa safi pia. Mabadiliko huanzia ndani na matokeo ndio yanayoonekana kwa nje. Mungu anapenda usafi. Mara nyingi alipotaka kukutana na wanadamu kama ni msomi wa Biblia kile kipindi cha Musa, alimwambia awaambie wana wa Israel wafue mavazi yao.
Hapa hakumaanisha mavazi ya kawaida. Alikuwa anasisitiza Usafi wa moyo yaani utakatifu. Kitu kisafi ni kitu kisichokuwa na doa lolote. Dhambi ni doa. Kumbuka dhambi ndiyo iliyomtenga mwanadamu na Mungu. Lakini kwa ajili ya usafi na Utakatifu wa Mungu alimtoa Yesu ili kuyafuta yale madoa yetu.
Mahali pengine anatulazimisha kuwa watakatifu. kwa kuwa yeye mwenyewe ni mtakatifu. Siku moja niliwahi kuwaambia watu fulani kuwa matokeo ya hali zetu za sasa ni madhihirisho ya hali za viroho vyetu. Kwamba kila kinachotokea physically tayari kilishatokea katika roho. Viroho vyetu vikiwa visafi hata muonekano wetu wa nje unakuwa nadhifu.
Hatua za kuchukua kwa haraka:
Kwanza ni lazima kijana ajitambue yeye ni nani na yupo kwa kusudi gani. Kujitambua ni hatua ya kwanza kabisa.
Pili, Aelewe jamii inayomzunguka inamhitaji. Inahitaji Nguvu zake. Inahitaji mchango wake. Kijana akishafahamu uhitaji wa jamii inayomzunguka, haitakuwa ngumu kwake kupata fursa.
Tatu, Bado una nafasi ya kurekebisha pale ulipoharibu. Mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa kuanguka sio tatizo. Tatizo ni pale unapoendelea kubakia pale chini.
Nne, Kijana awe na maono pamoja na malengo madhubuti.
Naamini utakuwa umejifunza mengi, na ninategemea mabadiliko makubwa sana. Nimalizie kwa msemo huu, "CHANGES IN OUR SOCIETIES DEPENDS THE CHANGES OF YOUTHS FIRST".
Nimependa kuirudia makala hii. Niliiandika miaka kadhaa iliyopita. Lakini nimeona kuna haja ya kuwakumbusha tena vijana wenzangu mambo haya.
Hakika tunahitaji kubadilisha mitazamo yetu ikiwa ni pamoja na mfumo wa maisha tunayoyaishi
Imeandikwa na,
Steven Mshiu
+255 655 882074
+255 768 882074
Barua pepe; smshiu42@gmail.comwww.inukauangaze.com

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni