Na Steven Mshiu
Kipindi fulani nikatembelea ofisi moja hivi kwa sababu nilikuwa nina shida na boss wa ofisi hiyo.
Kwa kuwa nilikuwa na vigezo vyote vya kuonana nae sikuwa na shaka yoyote, nilijua nitanyoosha njia moja kwa moja hadi ofisini.
Lakini jambo la kusikitisha wakati naingia getini tu, nilikutana na walinzi pamoja na maneno yaliyoandikwa "SIMAMA UKAGULIWE"
Sikuwa na ubishi wowote ingawa huyo boss alinifahamu, ilinibidi nisimame nikanyoosha mikono kando huku nimesimama wima, yule mlinzi akachukua kile kimashine chake na kufanya kazi ya ukaguzi,
Kwa bahati mbaya nilikuwa nimeweka ufunguo mfukoni, kile kimashine kikaanza kupiga alarm, nikaambiwa nionyeshe kuwa nimeweka nini mfukoni, Dah, ikabidi nitoe ule ufunguo,
Akanikagua mara ya pili tena.
Ndipo nikaruhusiwa kuingia ndani, kabla sijafika ofisini kwake nilikutana na Sekretari nae akanipa kitabu cha kujaza taarifa zangu na ninataka nini kwa huyo boss, ndipo akaniruhusu niingie.
Wanadamu tunaweza kujiwekea ulinzi mkubwa sana, unaposafiri ni lazima gari ikaguliwe na SUMATRA, wale mliosafiri kwa ndege mnafahamu ukaguzi wa pale uwanja wa ndege, Huwezi kuruhusiwa kusafiri bila kufanyiwa ukaguzi.
Hivyo basi katika safari hii ya mbinguni nayo ukaguzi wake haukwepeki, Ni lazima ufanye ukaguzi wa Roho yako kila siku, Huwezi kwenda mbinguni ilhali karoho kako ni kachafu.
Haijalishi unamfahamu MUNGU kiasi gani ni lazima kila siku ufanye ukaguzi wa roho yako. Huwezi kwenda mbinguni kama utakwepa ukaguzi wa roho yako.
#USIISHIE_NJIANI
#FIKIA_USHINDI_MKUBWA
Steven Mshiu
0655 882074
0768 882074
Email: smshiu42@gmail.com
Facebook page: m.fb.com/faithtz

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni