PASSWORD/NYWILA.
Na Steven Mshiu.
Dunia ya sasa imekuwa ni ya kujihami sana, Kila kitu ambacho mtu anafanya anasisitizwa kufanya kwa umakini na kwa usiri pasipo kumwamini mtu mwingine.
Ukienda benki kufungua akaunti utahitajika kuwa na Nywila imara kwenye kufanya miamala kwa kutumia kiotomotela, Nywila hizo ni siri kubwa sana kwako na kamwe huwezi kumwambia mtu, Ni siri yako.
Huduma zote za miamala ya simu kama M-pesa, Tigo pesa n.k nayo pia ni lazima uwe na password ambazo ni siri yako. Pesa ni zako ila kama huna password imara zisizoweza kudukuliwa na watu, huwezi kuzipata pesa hizo.
Dunia nzima imekuwa ni ya Password. Kuingia kwenye mitandao ya kijamii utahitajika kuwa na password, Ukitaka kuingia Facebook, kuna sehemu utahitajika kuweka password,
Simu zetu tumeweka password kuanzia upande wa sms, majina, file manager, yani kila kitu tumekiwekea password. Dhumuni la kuweka password ni kuhakikisha usalama wa simu zetu, kuhakikisha usalama wa taarifa zetu ili zisidukuliwe au kufahamika kwa watu wengine,
Unaweza ukasahau Warumi 6:1-3 inasemaje lakini huwezi kusahau password ya kuingia facebook
Unaweza ukasahau hata kuomba asubuhi kumshukuru Mungu kwa kukuamsha tena, Lakini huwezi kusahau password ya kuingia whatsapp kuangalia ni kitu gani kimetupiwa kwenye lile group.
Maisha yetu nayo yanahitaji password. Shetani anakesha usiku na mchana kuhakikisha anayadukua maisha yetu, kama huamini soma Ayubu 1, alijaribu kuyadukua maisha ya Ayubu lakini akamkuta ana NYWILA imara.
Alipojaribu kudukua maisha ya Yesu kwenye Mathayo sura ya nne, alimkuta Yesu akiwa Na NYWILA imara,
PASSWORD ya muhimu kwa maisha ya mkristo yeyote ni NENO LA MUNGU pamoja Na MAOMBI. Password hizi ni lazima ziwe imara sana zisizoweza kudukuliwa na yeyote.
Sasa wewe kuwa bize kuweka password, kuanzia twita, insta, fb, BBM, sijui na wapi tena Halafu sahau kuwekea maisha yako PASSWORD.
Kumbuka password zaweza kudukuliwa, Ni lazima uwe na password imara,
Neno la Mungu liwe imara kwenye maisha yako.
Maombi yako ni lazima yawe imara.
Mungu akubariki sana.
Steven Mshiu.
0655 882074
0768 882074
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni