Jumatano, 19 Aprili 2017

DHAMBI INA ASILI YA UPOFU.
Na Steven Mshiu.
Nakusalimu kupitia jina la Kristo Yesu. Ni siku nyingine tunapoianza wiki ambayo naamini itakuwa ya baraka sana kwako.
Kila siku tunajifunza na tutaendelea kujifunza maadam bado tupo hapa duniani hivyo ni lazima tujifunze.
Wakati fulani nikawa najiuliza inakuwaje hadi mtu anajikuta anatenda dhambi? Je hajui madhara ya dhambi? Kwamba dhambi inaondoa utukufu wa Mungu? Dhambi inasababisha ubaki uchi? Dhambi inakufanya wewe kuwa mtumwa? Licha ya kujua mambo yoooote hayo lakini wanadamu tunajikuta tumeshatenda dhambi. Kwanini? Dhambi ina asili ya upofu.
Jana wakati nafundisha somo la asubuhi kanisani kwetu katika kipindi cha UANAFUNZI NA MAANDIKO katika mafafanuzi yangu ndipo nilipoweza kupata majibu ya maswali niliyokuwa nikijiuliza. KWanini mtu anafahamu fika madhara ya dhambi lakini bado anatenda dhambi. Dhambi ina asili ya upofu.
Katika historia ya wana wa Israel, Mungu alikuwa akiwapiga na kuwaadhibu sana kwa sababu ya makosa ya kujirudia rudia. Kosa lao kubwa ni walishindwa kumtegemea na kumwamini Mungu. Mara nyingi walimwacha Mungu na kutegemea akili zao. Kipindi fulani wakiwa pale jangwani walianza kumlalamikia Musa kuwa aliwatoa Misri ili waje kufia pale jangwani. Hawakuona ule utmwa wa zaidi ya miaka 430 kule Misri. Hawakukumbuka jinsi Mungu aliliangamiza jeshi lote la Farao mbele ya macho yao. Kwanini? Dhambi ina asili ya upofu.
Pale walipotubu na kuomba rehema Mungu aliwarehemu. Pale walipopata ka ahueni kidogo wakajisahau tena. Unajua mwanadamu anapopata mafanikio kidogo mara nyingi humsahau Mungu. Wakati ambao mwanadamu anapopitia changamoto fulani huwa ni wakati wake wa kuwa karibu na Mungu sana. Lakini ile changamoto inapoisha hufikiri labda ni kwa sababu ya uwezo wake.
Baada ya taifa la Israel kupitia mateso mengi ikiwa ni katika utawala wa kuhani Eli na watoto wake ambao hawakutaka kuishi sawa na mapenzi ya Mungu. Hawakutaka kumsikiliza Mungu. Mungu akamwinua Samwel kuwa mwmuzi juu ya taifa hilo. Samweli akafanya kazi ya kuurudisha ule uwepo wa Mungu uliokuwa umeondoka. Akafanya maombi ya toba na rehema. Taifa la Israel likawa ktk raha kubwa ktk kipindi cha uamuzi wa Samwel. Mungu akapigana kwa ajili yao. Adui zao walipojipanga juu yao, Mungu aliwapiga kwa mvua ya mawe. Dhambi ina asili ya upofu.
Baada ya kukaa kwa raha muda mrefu kwny kipindi hiki cha Samwel. Ikumbukwe hapakuwa na mfalme. Kwani Mungu ndie aliekuwa mfalme. Israel wakaanza kutafuta sababu ya kumtenda Mungu dhambi. Wakamwendea Samwel wakitaka awafanyie mfalme ili wafanane na mataifa mengne.
Ili mtu atende dhambi huanza kuwa sababu zisizo na mashiko. Hawa wazee wanamwambia Samwel kwamba yeye amekuwa mzee na wanawe hawaendi ktk njia zake lakini lengo lao ni kumkataa Mungu kuwa mfalme wao. Wanataka mfalme atakaewaongoza ktk vita ili wafanane na mataifa mengine.
Ingawa Samwel aliwaambia mfalme wanaomtaka atakuwaje kwamba atawatumikisha, atawatesa, ataweka kodi kubwa, wao hawakusikia bali waliendelea kudai mfalme ili wafanane na mataifa mengine.
Hapa tayari walishatoka ktk mpango wa Mungu. Wanataka kufuata desturi za kidunia. Hawakukumbuka kuwa baba zao walipigwa kwa sababu hizo. Dhambi ina asili ya upofu.
Mtu mmoja akawa anafahamu fika kuwa kujenga nyumba juu ya mchanga ni lazima izolewe na mafuriko, lakini anajenga tu. Watu wanapomshauri kuwa asifanye hivyo yeye yuko bize kujenga. Matokeo yake anakuja kupata hasara kubwa zaidi.
Kijana leo unashauriwa usifanye hivi n kwa sababu dhambi imeshakupofusha unaendelea tu. Matokeo yake unakuja kufa kwa ukimwi. Wewe binti unashauriwa usicheze cheze na vijana kwanza ndo uko kidato cha tatu. Unafahamu fika unaweza kupata mimba, kwa sababu dhambi imekupofusha unaenda tu, mnakubaliana, mnafanya yenu, unapata mimba labda na ukimwi juu. Lakini tokea mwanzo ulifahamu madhara yake. Mwisho unajikuta ukiwa ktk hali mbaya zaidi.
Zipo dalili kadhaa zinazoonyesha kuwa mtu anakaribia kutenda dhambi.
• Kutotaka ushauri. Ukiona mtu hataki kushauriwa au hachukui hatua yeyote ile pindi anaposhauriwa hapo amefikia hatua mbaya zaidi ya kuangukia kwny dhambi.
• Kutafuta sababu. Ukiona mtu anatoa visababu sababu katka kumtumikia Mungu yupo kwenye hatari zaidi. Muda wa ibaada unapofika unaanza kutoa visababu vinavyokufanya usiende ibadani upo kwny hatari. Kilichowaponza Israel ni mambo kama haya haya.
• Kutaka kufanana na wengine. Mtu anapookoka huwa anabadilishwa moja kwa moja. Anakuwa milki y Mungu sasa anapotaka kufanana na wengine, hali hii husababisha nguvu zetu za kiroho kupotea.
Ukisoma katika kitabu cha 1 Samwel 8:1-22, ndipo utakutana na kisa hiki cha ajabu sana jinsi gani hawa watu walidhamiria kumkosea Mungu ingawa walishauriwa ila kwa sababu dhambi imeshawapofusha hawakuweza kubadilika.
Mpendwa mtu wa Mungu epuka kuwa mtumwa wa dhambi. Dhambi inakufanya uendelee kuumia na kuwa mtumwa.
Tubu leo na ukubali kubadilika.
Ubarikiwe.
©Steven Mshiu
0655-882074

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MAKUNDI MAWILI YA WATU WANAOKUZUNGUKA.

FAHAMU MAKUNDI MAWILI YA WATU KATIKA MAISHA YAKO. Na Steven Mshiu . Maisha ya kila mwanadamu yamezungukwa na watu. Watu hawa waweza kat...