Jumatano, 19 Aprili 2017

Kuokolewa kwa Neema

KUOKOLEWA KWA NEEMA.
Na, Steven Mshiu.
Wokovu wa mwanadamu ulianza kuandaliwa na MUNGU mwenyewe mapema pale bustanini Eden mara baada tu ya mwanadamu kumtenda Mungu dhambi na kuondoka katika uwepo wa Mungu.
Baada ya daraja la mawasiliano baina ya mwanadamu na Mungu kuvunjika, michakato mbalimbali iliweza kufanyika ilhali tu mwanadamu aweze kurudi katika mstari.
Mwanzo kabisa Mungu anamkamata mnyama asiyekuwa na hatia hata kidogo. Akamchinja ili kuwapatia wanadamu mavazi yatakayoficha ule utupu wao. Kumbuka dhambi inamfanya mtu kuwa mtupu yaani uchi. Unajua wokovu umetufunika. Yaani kuna mambo au vitu ambavyo vinatufanya tusionekane safi mbele za Mungu, hivyo kupitia wokovu ambao uligharimu uhai wa kitu umeweza kututakasa.
Lakini damu na ngozi ya yule mnyama havikuweza kukidhi mahitaji ya wokovu wa mwanadamu. Yote haya yalitokea katika Agano la Kale. Mungu alikuwa akiwapatia wokovu kupitia damu za wanyama.
Baada ya mambo yote haya, alitakiwa mtu atakae kuwa tayari kuyatoa maisha yake na uhai wake kwa ajili ya wanadamu na sifa za mtu huyo ni lazima awe mtu asye na hatia, mwenye upendo na atakaekubali kufa. Tena kifo cha msalaba.
hapakuonekana kiumbe chochote kile chenye uhai, mbinguni wala duniani kilichoweza kusimama na kusema kuwa atajitoa kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu. Ukimya mkubwa ukatanda mbinguni.
Katika Ukimya ndipo alipojitokeza mtu mmoja akasema kuwa yeye atakwenda kuyatoa maisha yake kwa ajili ya wanadamu, ili kupitia damu yake wanadamu tupate wokovu
Huyu ni YESU KRISTO mwana wa mfalme MUNGU. Hakuona kule kuwa mwana wa Mungu kuna thamani kuliko mwanadamu alieumbwa kwa mfano wa Mungu.
Hivyo akayatoa maisha yake kwa ajili ya kuwaokoa wanadamu.
Kwa sababu hiyo basi nakusudia kuanza kuandika kitabu kinachohusu "MAMBO TISA YANAYOKAMILISHA WOKOVU".
Nitafurahi sana kupata mchango wako na mawazo yako ili kuweza kukifanya kitabu hicho kuwa bora zaidi. Najua sote tunatamani kuufahamu wokovu wetu na gharama zake ili tuweze kufika mbinguni.
Kama utakuwa na mchango wowote tafadhali waweza kunitumia ktk inbox yangu ya Facebook, au kupitia E-mail smshiu42@gmail.com
Au kupitia simu ya mkononi namba 0655-882074 na 0768-882074
Naamini tutashirikiana vyema katika kuujenga mwili wa Kristo.
Mungu akubariki sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MAKUNDI MAWILI YA WATU WANAOKUZUNGUKA.

FAHAMU MAKUNDI MAWILI YA WATU KATIKA MAISHA YAKO. Na Steven Mshiu . Maisha ya kila mwanadamu yamezungukwa na watu. Watu hawa waweza kat...