Jumatano, 19 Aprili 2017

KULEWA MADARAKA.
Na, Steven Mshiu
Leo napenda tuangalie hili suala la madaraka. Madaraka ni mfumo wa Mungu mwenyewe aliounzisha huko mbinguni yeye mwenyewe. Mungu yeye mwenyewe mi mwenye madaraka na hufuata protoko yaani husimamia kanuni zake za kiuongozi na utawala.
Kiongozi yeyote anaesimama na kuliongoza taifa lolote, hupewa mamlaka na maongozi kutoka kwa Mungu. Hivyo ni vyema kuitii na kuiheshimu kila mamlaka iliyopo. Sisi hatuna mamlaka ya kumhukumu kiongozi yeyote anaesimama mbele yetu hata kama amekosea kiasi gani. Yupo Mungu aliemuweka ndiye anaeweza kumhukumu. Biblia inatuagiza hivyo.
Leo nataka nikuletee kisa kimoja cha mtu alieitwa Sauli. Sauli alichaguliwa na kutawazwa na Mungu ili awe mfalme juu ya taifa la Israel. Mtu huyu alitoka ktk jamii ndogo sana ya Israel yaani alikuwa ni jamaa ya Benyamini.
Baada ya wana wa Israel kukosa mfalme na mwamuzi juu yao kwa muda mrefu sana tangu kipindi cha Samsoni ndipo wakamwambia Samwel awatafutie mfalme atakaewaongoza ktk vita. Nyakati hizo taifa hili teule la Mungu lilikuwa limemsahau Mungu kabisa. Hawakutambua mamlaka na madaraka ya Mungu kuwa ni tofauti na ya dunia hii
Hawakukumbuka aliewaongoza jangwani pindi walipotoka Misri. Hivyo wakawa wanataka mfalme. Ndipo Mungu alipomwinua Sauli.
Baada ya Sauli kuinuliwa na kuwa mfalme juu ya Israel, akaota pembe. Akajisahau ya kwamba ametoka ktk jamii ndogo sana ya Benyamini. Akasahau kuwa alipakwa mafuta illi aliamue taifa teule la Mungu. Akaacha kumsikiliza mchungaji wake Samwel. Akajipa cheo cha Mungu. Akajiona kama yeye ni mungu wa israel. Akafanya kama alivyoweza.
Siku moja Bwana Mungu akampa Samweli maelekezo kuwa amwambie Sauli aende awapige Amaleki na kuharibu kabisa kila kitu cha hao Amaleki maana waliwatesa sana Israel walipokuwa wakitoka Misri. Tena asiache mfugo hata mmoja wa hawa Waamaleki.
Sauli hakutaka kuyasikia hayo maneno na maagizo ya Mungu kupitia kwa Samwel.
Sauli akatoka akaandaa jeshi kuishukia Amaleki. Akajifanya mwema sana. Akawaambia Wakeni waliokaa Amaleki kuwa waondoke asije akawaua pamoja na Amaleki. Akaanza kuipiga Amaleki. Akawaona kondoo na ng'ombe walionona akawaacha. Akamkamata mfalme Agagi, mfalme wa Waamaleki na kumwacha hai.
Lakini mtu huyu alipewa maagizo kuwa asiache kitu hata kidogo. Wala hakuyatii maagizo hayo. Akafanya kwa maamuzi yake.
Mungu akanena na Samweli kwa mara nyingine kuwa anajuta kwa sababu alimtawaza ili awe mfalme maana amerudi nyuma wala asimfute Mungu. Wala hakufanya yale aliyomwamuru. Kwa hiyo Mungu akamkataa kabisa Sauli. Ni kwa sababu alilewa madaraka.
Sauli alipoulizwa kwanini hakutii maagizo ya Mungu, yeye alijitetea kuwa ametii na amewachukua hao wanyama ili waje kumtolea Mungu sadaka. Mara ni wale watu ndio waliowaacha hao kondoo. Yeye hakusimama ktk nafasi yake. Hakuambiwa amwache Agagi akiwa hai. Hili likawa ni kosa kubwa sana mbele za Mungu.
Hivyo Mungu akamwacha Sauli kabisa. Tena akamkataa. Yote haya ni kwa sababu alilewa madaraka.
Siku za leo kuna watu ambao Mungu amewadhamini na kuwapa kanafasi kadogo tu ka uongozi lakini wanautumia vibaya. Kumbuka uko kwa niaba ya Mungu. Tumia mamlaka yako vizuri. Watendee wananchi haki. Tafuta kuyafuata maagizo ya Mungu. Viongozi wa dini wana nafasi kubwa sana ktk nafasi yako ya uongozi. Ni vyema kuwasikiliza. Wao ni sauti ya Mungu. Wao ndio kina Samwel wa leo. Ndipo utakapoona mafanikio makubwa ktk mamlaka uliyopewa.
Kisa hiki sio mimi niliyetunga. Ni maandiko halisi kutoka katika Biblia. Kisa hiki kwa wale wasomaji wa Biblia kinapatikana ktk kitabu cha 1 Samwel 15:1-34.
Tumia nafasi unayoipata kwa umakini.
Mungu akubariki sana.
0655 882074

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MAKUNDI MAWILI YA WATU WANAOKUZUNGUKA.

FAHAMU MAKUNDI MAWILI YA WATU KATIKA MAISHA YAKO. Na Steven Mshiu . Maisha ya kila mwanadamu yamezungukwa na watu. Watu hawa waweza kat...