MATOKEO MABOVU YA
KUTOTII SAUTI YA MUNGU.

Wakati Eli alipotoka nje ya kusudi la Mungu, akafanya kama
alivyoweza ndani ya hekalu, akaacha kuwalea watoto wake ktk maadili ya kiroho,
wakalichezea hekalu la Mungu, wakafanya dhambi na uchafu wa kila namna kama
walivyoweza bila kuulizwa chochote na baba yao Eli. Ndipo hasira ya Bwana
ilipowaka juu ya Eli na wanawe. Mungu akaacha kuongea na Eli, kwa sababu hakuwa
anayafuata maagizo yake tena. Na wakati huu neno la Mungu lilikuwa adimu sana
ktk Israel. Kwa sababu bado Mungu alikuwa analipenda taifa la Israel, ndipo
alipoanza mpamgo wa kumtafuta na kumwandaa Samwel kuichukua nafasi ya Eli. 1
samwel 2:35, Sikio la kufa siku zote huwa halisikii dawa. licha ya unabii wote
huu bado Eli hakuweza kutubu wala kufanya juhudi za kulirejeza hekalu na taifa
ktk hali ya utakatifu wa Mungu.
Mungu anaposema na Samwel juu ya dhambi ya Eli, anaanza
kumwambia yatakayompata Eli pamoja na familia yake. 1 Samwel 3:11-14. Tayari
Mungu alishamkataa moja kwa moja. Hapa anasema mambo makubwa na mabaya
yatakayompata Eli na familia yake. Hakuna kitu kibaya kama kukataliwa na Mungu.
Mungu anapokukataa kifo ni lazima kiwe nyuma yako. Na hatua ya kwanza unaanza
kudhoofika kiroho. Kifo cha kimwili kama kinavyoonekana ktk 1 Sam 4:11,19 ni
matokeo ya kifo cha kiroho.
Jambo lingine ni utukufu wa Mungu kuondoka. Mungu anakaa
pale ambapo utakatifu wake unaenziwa. mahali ambapo anaposema watu wanaisikia
sauti yake. Lakini wakati dhambi inapoingia tu basi utukufu wake huondoka. 1
Sam 5:1-2.
Yapo matokeo meeengi yanayotokana na kutoitii sauti ya
Mungu. Kuna wakati hata wewe Mungu alisema nawe kuhusu kufanya jambo fulani, na
unaweza ukawa ni shahidi wa kilichotokea kama ulitekeleza au la. Ni vizuri
kutii na kufanya kile anachotuagiza Mungu ili aendelee kuwa pamoja nasi. Yeye
anampenda mtu mti na mnyenyekevu anaeisikia sauti yake na kufuata maagizo yake.
Naibariki asubuhi yako na Mungu awe pamoja nawe kwa kila
unalolifanya linalomletea utukufu.
Steven Mshiu
+255 655 882074
+255 768 882074
smshiu42@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni