MTAZAMO WA MUNGU NA
MTAZAMO WA WANADAMU.
------------------------------------------------------------------
Na, Steven Mshiu
Nakusalimu kupitia jina la Kristo Yesu ambaye ni Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Ni matumaini yangu kuwa bado una uzima wa kutosha. Nina kila sababu ya kumtukuza Mungu kwa hilo.

Tumekuwa busy sana kwa mambo
mbalimbali, hadi kukosa muda wa kuweza kuweka
makala katika blog hii, ni kwa sababu tunaandaa mipango mizuri ya kuhakikisha blog hii inakuwa bora zaidi. Tumeshapata walimu kadhaa wa Neno la Mungu, na mapema tu utajifunza mengi, utahamasika kwa mengi kupitia blog hii. Lengo letu ni kuihubiri injili ya Kristo inayoleta wokovu kwa wanadamu. Ndicho kiini cha blog hii.

Leo napenda nikuletee makala hii fupi. Nafikiri
itakuhamasisha na kukupa morali wa kuamini kuwa kile Mungu alichokisema
juu ya maisha yako ni lazima kitimie haijalishi ni kwa muda gani. Unajua wanadamu tuna mtazamo, na Mungu pia ana mtazamo. Wewe waweza kuona hivi, Mungu akaona vile. Hivyo kuna tofauti kubwa sana kati ya mtazamo wa MUNGU na wa wanadamu.

Nikuletee kisa kimoja kwa leo ndani ya Biblia kinachomhusu
mmoja wa watoto wa YAKOBO mwana wa ISAKA Ambaye ni uzao wa ahadi ya MUNGU kwa
IBRAHIMU. Alikuwa ni mtoto wa 11 katika uzao wa Yakobo na kifungua mimba katika
tumbo la Rahel, nduguye Leah. Kumbuka Isaka alikuwa na wake wawili (Lea na
Rahel). Jina lake aliitwa YUSUFU.
Yusufu alikuwa ni mwana wa uzee kwa Yakobo, hivyo kwa kiswahili chepesi, baba yake alimdekeza sana, kama yeye(babaye)
alivyodekezwa na mamaye Rebeka.
Yusufu alikuwa ni mwana wa uzee kwa Yakobo, hivyo kwa kiswahili chepesi, baba yake alimdekeza sana, kama yeye(babaye)
alivyodekezwa na mamaye Rebeka.
Mtazamo wa Yakobo kwa
Yusufu alimtazama kama mpelelezi wa
nduguze, maana kipindi fulani alikuwa akienda kuwatazama nduguze makondeni
na kumletea babaye habari. Mwanzo 37:2-3.
nduguze, maana kipindi fulani alikuwa akienda kuwatazama nduguze makondeni
na kumletea babaye habari. Mwanzo 37:2-3.
Kwa ndugu zake, mtazamo wa ndugu zake Yusufu, walimtazama
kama ni kiherehere, mmbea na mnafiki, hivyo wakamchukia Mwanzo 37:4 Haikuishia
hapo.
Waishmaili wakamtazama Yusufu kwa mtazamo wa kibiashara.
Hivyo wakamnunua Yusufu, Mwanzo 37:27-28 Kwa kuwa wa- Ishmaili walikuwa ni
wafanyabiashara, na wameshapata dili jepesi hivyo wakamuuza tena kwa wafanyabiashara
wengine wakubwa ambao ni wa-Midian. Na wa-Midian nao wakamuuza tena kwa POTIFA.
N.B: Kumbuka hii ni mitazamo ya wanadamu juu ya YUSUFU,
Lakini Mungu alishamtazama kivingine, hivyo kote huku anakopitia mtazamo wa
Mungu uko pale pale. Kwa Potifa. Potifa akamtazama YUSUFU kama mlinzi wa nyumba
yake maana alikuwa mwaminifu sana. Mwanzo 39:4-5 Lakini bado mitizamo ya
wanadamu haiishi. Mke wa POTIFA akamtazama kwa mtaza.mo wa tamaa. Yaani mtazamo
wa kimapenzi, kwa kuwa alikuwa ni kijana mzuri, body yake iko safi. Hivyo
akamtamani Mwanzo 39:6b-7. Na kwa sababu kijana huyu asieijua dhambi alikuwa
akilinda utakatifu wake na mtazamo wa MUNGU kwake, hivyo hakutenda dhambi
yoyote.
Katika kukimbia kwake akaangukia gerezani, mle gerezani
wakamtazama kama ni mhalifu mkubwa sana. Maana alifungwa katika gereza la
mfalme. Mwanzo 39:20, Mkuu wa gereza naye akamtazama Yusufu
kama msimamizi wa wenzake 39:21 Wakati wa MUNGU kudhihirisha jinsi anavyomtazama YUSUFU ulipofika, hakuna hata mmoja alieweza kuubadilisha.
kama msimamizi wa wenzake 39:21 Wakati wa MUNGU kudhihirisha jinsi anavyomtazama YUSUFU ulipofika, hakuna hata mmoja alieweza kuubadilisha.
Akiwa gerezani, ndipo mtazamo wa Mungu ulipoanzia safari ya
kutimia. Miongoni mwa wafungwa wa mfalme, wawili wanaota ndoto, na Yusufu
anawatafsiria. Kutokana na tafsiri ya Yusufu, yakawa ya kweli. Farao akaota
ndoto ambayo ilimnyima usingizi na hapakupatikana mtu wa kuitafsiri.
Yule mfungwa mmoja akamkumbuka Yusufu alivyomtafsiria ile ndoto yake, akapeleka ombi kwa farao, kuwa kuna mfungwa/mhalifu mmoja wa kiebrania katika gereza la mfalme anaweza
kuitafsiri ndoto yako. Yusufu akaitwa mbele ya Farao na kuitafsiri ndoto. Hakika ikawa ni ya kweli.

Soma Mwanzo sura ya 41. Yusufu akapata kibali mbele ya
Farao. Mwanzo 41:37-40. MUNGU
ALIMTAZAMA YUSUFU KAMA MTU WA TATU KTK TAIFA LA MISRI. Kwa lugha nyingine ni kwamba Mungu alimtazama
kama WAZIRI MKUU. (Mwanzo 41:41-42). Wakati wa kuinuliwa kwa Yusufu ukafika. Muda hautoshi kuendelea kuandika mengi, ila nina haya ya kuandika,

Wanadamu wanaweza
wakakutazama kama kahaba/malaya fulani hivi, lakini Mungu akakutazama kama mama/baba bora wa familia. Wanaweza wakakutazama kama
jambazi/mwizi fulani hivi lakini Mungu akakutazama kama mtumishi wake. Wanaweza wakakutazama mtumwa lakini Mungu akakutazama kama mfalme.
Wanaweza wakakutazama kama
asie na mwelekeo lakini Mungu akakutazama kama kiongozi mkubwa. Wanaweza wakakutazama kama masikini lakini Mungu akakutazama kama tajiri. Wanaweza wakakutazama kama
wewe ni wa kufa tu lakini Mungu akakutazama kama mtu wa kuishi. MTAZAMO WA MUNGU NI TOFAUTI KABISA NA MTAZAMO WA WANADAMU.

Walimtazama Daudi kama kijana mdogo, tena mchungaji wa kondoo
tu, ambaye hayawani wanaweza kuila nyama yake. lakini Mungu alimtazama kama
shujaa na Mfalme wa Israel. Wanadamu wasikutishe na
mitizamo yao.
Nimalizie kwa kukumbusha mambo
machache.
shujaa na Mfalme wa Israel. Wanadamu wasikutishe na
mitizamo yao.
Nimalizie kwa kukumbusha mambo
machache.
*Ili mtazamo wa Mungu utimie ktk maisha yako ni lazima
uuishi huo mtazamo. Mwanzo 39:9.
*Dhambi ni kikwazo kikubwa cha mtazamo wa Mungu kutimia.
Amuzi 16:17-20
*Pale mtazamo wa Mungu unapotimia usilipe kisasi kwa
wanadamu waliokuwa na mtazamo tofauti juu yako. Mwanzo 48:8-21
*Mtangaze Mungu wako kuwa yeye ndie mwezeshaji wa kila kitu.
Nikushukuru kwa kusoma ujumbe huu mfupi. Ni maombi yangu
Mungu akakuinue na kutimiza kile alichoahidi katika maisha yako.
Ahsante.
Kama utakuwa na maoni au ushauri, unaweza kuwasiliana
na mwandishi wa makala hii,
Imeandikwa na Steven Mshiu,
0655-882074, 0768-882074
baruapepe smshiu42@gmail.com
Ahsante.
Kama utakuwa na maoni au ushauri, unaweza kuwasiliana
na mwandishi wa makala hii,
Imeandikwa na Steven Mshiu,
0655-882074, 0768-882074
baruapepe smshiu42@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni