UMEPAKWA MAFUTA KWA
AJILI YA KAZI MAALUM. HUNA NAMNA YA KUYAKWEPA MAJARIBU. HEBU HAYO MAJARIBU YAWE
NI DARASA KWAKO.
...............................................................................................................................
Na, Steven Mshiu.
Habari mpendwa rafiki,
Naamini Mungu anakutunza vyema,
Ninawiwa kutoa shukrani zangu za dhati kwako wewe ambaye kupitia makala ninazoziandika humu mtandaoni na kwenye blog zetu zimekuwa msaada kwako.
Kama unavyofahamu sote tu viungo katika mwili wa Kristo. Hivyo ni vyema kujengana na kutegemezana. Sote tunategemeana ili kuujenga mwili wa Kristo ili tuweze kuufikia ufalme wake.
Unapotenga muda wako kusoma makala hizi naamini kuna kitu Mungu anaenda kukutendea. Nikutaarifu tu kuwa kabla ya kuandika chochote humu huwa namuomba Mungu anijalie hekima Na ujumbe utakaokuwa ni wa muhimu kwa mhitaji.

Leo napenda nikuletee mambo machache tu. Hivi unafahamu
kabla hujazaliwa tayari Mungu alishakupangia majukumu au kazi maalum
utakayokuja kuifanya hapa duniani?
Katika Yeremia 1:4-7, tunaona ni jinsi gani ilivyomsumbua Yeremia kutambua kuwa yuko kwa ajili ya kazi maalum. Mungu anamwambia kabla hajazaliwa alikwisha kumchagua Kwa kazi maalum Kama inavyojieleza kwenye mistari inayofuata.

Hata wewe una kazi maalum. Hata mimi ninayo pia.
Baada ya Mungu kumkataa Sauli, sio kwamba utendaji wa Mungu ungekomea pale. Bado Mungu alikuwa ana mpango mzuri juu ya taifa la Israel. Kwa wale wasomaji wa Biblia watakumbuka kuwa Mfalme Sauli hakuwa ni chaguo la Mungu kwani alikuwa ni chaguo la wanadamu. Hivyo hakuona umuhimu wa kuyashika maagizo ya Mungu. Ndiyo sababu kubwa ya kukataliwa. Soma 1 Samwel 15:

Kwa kuwa Sauli hakuwa ni chaguo la Mungu, na kwamba tayari
chaguo la wanadamu limekwama, Mungu anajipatia chaguo lake katika nyumba ya
Yese mtu wa Bethlehem. Kijana mdogo, tena mtoto wa mwisho wa mzee Yese. Mungu
anamtaka yeye awe Mfame. Matendo 13:22, Mungu anajisifia kwa kijana Daudi Kuwa
yeye anaupendeza moyo wake na atafuata maagizo yote atakayoagizwa na Mungu.
Majukumu ambayo anatakiwa kuyakabili sio madogo. Tayari
taifa la Israeli lilikuwa limeshambuliwa na maadui wengi. Wafilisti ndio
walikuwa maadui wakubwa sana wa taifa hili teule la Mungu. Hivyo alitakiwa
akabiliane nao na alete ushindi mkubwa. Sio Wafilisti tu. Mfalme Sauli naye
angekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa Daudi. Kwani ile nafasi yake kama Mfalme
ndio inachukuliwa na kijana Daudi badala ya mwanae Yonathan. Bado ndugu zake
waliomtangulia wangeweza kuwa ni jaribu kwake. Yaani kwa nini yeye ni mdogo
halafu anakiwa awe mfalme??
Kwa kuwa Mungu alikuwa ndiye mpangaji wa mambo yote
alifahamu fika kuwa Daudi asingeweza kukabiliana na majaribu hayo yoooote bila
kutiwa mafuta. Ndipo Mungu anamugiza Samwel akamtie mafuta kwa ajili ya kazi
ambayo ipo mbele yake.
Nataka tujifunze jambo moja au mawili ya muhimu hapa. Chaguo
la Mungu ni tofauti na la wanadamu kabisa. Nakukumbuka kipindi cha nyuma
niliwahi andika makala moja inayosema "MTAZAMO WA MUNGU NI TOFAUTI NA
MTAZAMO WA MWANADAMU". Kuwa mwanadamu yeye anaweza kuangalia Kwa nje tu na
kutoa hukumu (judge) lakini Mungu huangalia moyo na ile hali ya ndani ya mtu.
Hivyo basi wakati amefika katika nyumba ya Yese, Yese
aliweza kuwaita wanawe wote ili wapite mbele ya Samwel, Akamwacha Daudi ambaye
kwa wakati huo alikuwa akichunga mifugo ya baba yake. Wao walimtazama kwa
mtazamo wao kama wanadamu kwanza ni mdogo, halafu hana hata uzoefu wa vita.
Kumbe ndie aliyekuwa chaguo la Mungu. Na kweli walipopita wote ya Samweli
hakuonekana hata mmoja. Soma 1Samwel 16:1-13. Yese anaulizwa je wanao wote wako
hapa??? Anasema ndio ILA kuna mmoja tena mdogo wao yuko machungani. Daudi
alipokuja kweli akawa ndiye ambaye Mungu alikuwa amemchagua. Naye Samweli
AKAMTIA MAFUTA
Mara nyingi Mungu huinua vile vinyonge ili kuviaibisha
vyenye nguvu. Daudi huyu ndiye atakaekuja kumuangusha Goliath ambaye Mfalme
Sauli na wengine wamemshindwa. Mungu alimwinua Yusuph alieonekana ni mwota
ndoto tu, mtumwa na mfanyakazi wa kazi za ndani kuja kuwa WAZIRI MKUU, lakini
ni baada ya kupitia majaribu mengi ambayo yalikuwa ni darasa kwake na kuweza
kuitimiza ndoto yake.
Kupakwa mafuta ni ishara ya Roho Mtakatifu. Yesu akawaambia
wanafunzi wake kuwa wasitoke pale walipokuwa wamekusanyika hadi watakapopokea
nguvu. ambayo italetwa na Roho Mtakatifu. Ndipo watakapoweza kuwa mashahidi
wake. Matendo 1:8, Huyo Roho ndiye atakaewawezesha maana kwa nguvu zao
wasingeweza. Yapo majaribu meengi ambayo yalikuwa mbele zao na pasipo Roho
Mtakatifu wasingeweza kuvumilia.
Yesu akiwa amefunga siku arobaini hali akijawa na Roho mwovu
alipokuja na kunjaribu hakika aliweza aliweza kumshinda. Kwanini. Kwa sababu
ROHO MTAKATIFU tayari alikuwa ndani yake. Mathayo 4:1-12, Stefano akiwa amejawa
Roho, anapigwa kwa mawe hadi kufa huku akimshukuru Mungu, na kuwaombea rehema
waliokuwa wakimpiga mawe. Asingeweza kuvumilia kama alikuwa hajapakwa mafuta ya
Roho Mtakatifu. Yesu asingeweza kuvumilia kifo cha aibu. Kifo cha Msalaba kama
Hakuwa na mafuta haya Ya Roho Mtakatifu
Daudi naye asingeweza kupambana na majaribu yaliyokuwa mbele
yake dhidi ya Sauli Kama hakuwa na Mafuta haya. Asingeweza kupambana na Goliath
aliyekuwa tishio kwa akina Yonadabu na Israel kwa ujumla kama hatakuwa na
mafuta Haya yaani Roho Mtakatifu.
Hata sisi leo hatuwezi kukabiliana na majaribu ya dunia hii
kama hatuna mafuta haya. Hatuwezi kufanya chochote pasi kuwa na uongozi wa Roho
Mtakatifu. Sehemu fulani katika Biblia inasema kuwa "Wanaoongozwa na Roho
ndio wana wa Mungu. Akasema tena katika Warumi 8:26, Kuwa sisi hatuwezi kuomba
ipasavyo, ila Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkika. Mambo mengi tu
hatuwezi peke yetu pasipokuwa na msaada wa Roho Mtakatifu.
Hapo kazini kwako kuna watu wengi tu wanaimezea mate hiyo
nafasi yako.
Kuna watu wanaimezea mate familia yako. Wanammezea mate mume wako. Wanammezea mate mke wako
Wanammezea mate huyo mchumba wako.
Wanaimezea mate biashara yako.
Wewe kama wewe huwezi kwa nguvu zako. Unamhitaji Roho Mtakatifu atakaekuwezesha katika yote. Sauli alijitahidi kutumia nguvu zake matokeo yake alishindwa vibaya.

Sote tunamhitaji Roho huyu. Maana tunaishi katika dunia
ambayo ina kila aina ya majaribu.
Hayo ni kwa uchache tu. Ningeweza kuandika mengi lakini nataka tu uone umuhimu wa Roho Mtakatifu katika kila unachokifanya.
Binafsi kila siku huwa kila siku ninamuomba Mungu anijaalie na anipe Roho wake aniongoze juu ya kitu.

Na ukiona unapata hasara kwenye kila kitu unachokifanya
tambua fika kabisa hujamhusisha Roho Mtakatifu
Mungu akubariki kwa ujumbe huu mfupi.
Mungu akubariki kwa ujumbe huu mfupi.
Kama utakuwa na maoni au chochote, usisite kuwasiliana nami.
Naamini pia yuko Roho Mtakatifu anaeweza kukufundisha mengi zaidi.
Ahsante.
Naamini pia yuko Roho Mtakatifu anaeweza kukufundisha mengi zaidi.
Ahsante.
Makala hii imeandikwa na Steven Mshiu,
Mwandishi, mwalimu na mshauri juu ya masuala ya kiroho na kumjua Mungu
0655-882074
smshiu42@gmail.com
Mwandishi, mwalimu na mshauri juu ya masuala ya kiroho na kumjua Mungu
0655-882074
smshiu42@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni