Ijumaa, 28 Julai 2017

BADILI NAMNA YA KUFIKIRI

BADILI JINSI YA KUFIKIRI.

Na Steven Mshiu
Moshi, Tanzania.

Habari mpendwa rafiki. Naamini umeamka vyema na tayari umeshayaanza majukumu yako ya kila siku. Na kama bado hebu fanya haraka, maana muda haukusubiri hata kidogo.

Leo nataka tukumbushane mambo kadhaa. Hivi unaahamu kama fikra na mawazo yetu ndiyo yaliyotufikisha hapa tulipo? Kile unachokiwaza au ulichokuwa ukikiwaza kwenye akili yako ndio matokeo unayoyaona leo.

Kuna vitu ambavyo tulikuwa tukivifikiri pindi tulipokuwa wadogo, lakini kadri siku zinavyokwenda haviwi kama tulivyokuwa tukifikiri. Vinabadilika na kutufanya nasi tubadili namna ya kufikiri.

Kipindi nikiwa na umri wa miaka minne, Hapo nimeshaanza kupata akili kidogo. Siku moja nilisafiri nikiwa nimeambatana na bibi yangu ambaye kwa sasa ni marehemu. Ilikuwa ni safari ndefu kidogo. Hivyo ilitulazimu kutumia usafiri wa gari la abiria aina coaster.

Kwa kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kupanda gari nilifurahi sana. Nilitamani kujifunza mambo mengi sana kupitia safari ile. Bibi yangu alitumia muda mwingi kunitajia majina ya maeneo na vituo kadhaa wakati tukiwa ndani ya gari lile. Kwakweli nilikuwa makini sana kumsikiliza ili na mimi nivielewe vituo vile.

Wakati safari ikiendelea mimi nikiwa ndani ya gari nilishangaa jambo moja tuu, Binafsi lilinisumbua sana akili maana halikuwa jambo la kawaida kabisa kwangu.
Nilishangaa kuona miti, nguzo za umeme, na baadhi ya mabango vikirudi nyuma tena kwa kasi.

Kwa kuwa sikupenda kuuliza kwanini inakuwa hivi mimi nikajiaminisha kuwa kumbe ukiwa ndani ya gari miti nayo hutembea. Nikaamini hivyo, na hata kama ningekutana na mtu akaniuliza basi ningemjibu hivyo.

Hatimaye tukafika kule tulipokuwa tukielekea lakini mimi tayari namna yangu ya kufikiri ni kwamba miti nayo hutembea. Lakini jambo lililoendelea kunichanganya akili ni wakati tunarudi kutoka kule safarini, nilishangaa kuiona tena ile miti ikirudi kule tulipotoka kwa kasi ile ile. Hapa ikabidi niulize.
Eti bibi, Mbona wakati ule hii miti ilikuwa inarudi nyuma kwa kasi, na sasa tumekutana nayo tena inarudi kwa kasi?
Ina maana miti nayo husafiri?

Akaniambia mjukuu wangu miti, wala hizo nguzo za umeme hazisafiri wala hazijahama pale zilipo. Kinachofanya uone kama miti nayo hutembea ni hii gari uliyopanda ndiyo inayotembea. Hapo ndipo namna ya kufikiri kwangu, na kuona kumbe nilikuwa nafikiri tofauti na namna inavyotakiwa kuwa. Hivyo bibi yangu akawa amebadilisha namna ya kufikiri kwangu. Tangu siku hiyo sijawahi kufikiri tena kuwa miti nayo hutembea.

Nataka nikukumbushe mambo haya ya msingi, huenda yakawa msaada kwako. Sote tuna namna ya kufikiri, Na kila mtu kuna jambo ambalo kwake analiona ni sahihi au yuko sahihi kifikra. Sawa sijakataa. Ila ni vyema ukainyambua akili yakili yako ikupe majibu je hicho unachokiwaza kipo sahihi? na kama hakipo sahihi ni hatua gani uchukue kuhakikisha kuwa kinakuwa sahihi?

Kama mimi nisingemuuliza bibi yangu yawezekana hadi leo ningekuwa naamini kuwa miti nayo hutembea. Unapoziamini fikra zako tu bila kutaka kujifunza ni kutafuta kupotea. Biblia inasema tutafute maarifa. Maarifa hayapatikani bure bure tu. Hupatikana kwa kujifunza.

Dunia inabadilika, na mambo nayo yanabadilika. Kama utabaki na fikra ulizokuwa nazo miaka mitano iliyopita, utaiona dunia kama sio mahali sahihi kwako kuishi. Kipindi kile tunauziwa sukari kilo moja kwa shilingi 800 lakini leo tunanunua kilo moja kwa shilingi 2500 hadi 3000, Ni lazima tubadili fikra zetu kutoka 800 hadi 3000.

Kama ulikuwa unafikiria kutengeneza kipato cha elfu kumi miaka hiyo, Hivi sasa ni lazima ubadili zile mbinu ulizokuwa ukizitumia kutengeneza elfu kumi, ufikiri mara mbili yake.

Kufikiri kwako ndiko kutakufanya ufanikiwe ama usifanikiwe. Uinuliwe ama usiinuliwe. Mtu mmoja akawa ananiambia eti wale ambao wako bize wanasema wanamtumikia Mungu ni kwamba wamekosa kazi ya kufanya. Nikamjibu unatakiwa kubadili namna ya kufikiri. Nikamuuliza mbona wewe huna mafanikio yoyote. Akaniambia eti hali ya maisha ni ngumu. Magufuli amebana. Nikamwambia pole sana. Fikra zako na mawazo yako ndio yamekufanya uwe jinsi ulivyo.

Yesu alipotaka kumponya mtu jambo la kwanza alianza kumbadilisha yule mgonjwa fikra zake. Alipokutana na mtu aliyekuwa pale birikani kwa miaka 38, akamuuliza unataka kupona? Yule mgonjwa fikra zake zilikuwa kwa malaika tu, kwamba pale maji yanapotibuliwa na malaika, basi mtu mwingine huwahi kule birikani na kupona ugonjwa wake.

Lakini Yesu hakuwa anahitaji maelezo yote hayo. Yeye alitaka jibu moja tu kutoka kwa mgonjwa yule kuwa "NDIO NATAKA KUPONA". Pale alipobadili namna ya kufikiri kuwa hakuna njia moja moja tu ya kupata uponyaji na akamuamini Yesu, Yesu akamwambia beba godoro lako na uende. Mara yule mtu akawa mzima.

Ningeweza kukuletea habari nyingi za watu ambao Yesu aliwatendea miujiza lakini ni baada ya kubadili namna zao za kufikiri.
Naamani alikuwa akifiri kuwa ukoma wake utapona baada ya kuwekewa mikono na nabii Eliya, Lakini anaambiwa akaoge Mto Yordan mara saba, alipobadili namna ya kufikiri kutoka kuwekewa mikono na kwenda kuoga Yoradan mara saba akapokea uponyaji.

Mitume wa Yesu walinogewa na mikate kipindi walipokuwa pamoja na Yesu, Hawakuelewa kuwa kuna wakati Yesu atawaacha, Yesu alipowaacha tu, ndipo akili zao zilipobadili namna ya kufikiri na kutambua majukumu yao. Wakaanza kuihubiri injili.

Mpendwa rafiki,
Nakukumbusha kuwa kuna siku hutakuwa hapo ulipo. Kile unachokitegemea hakitakuwepo. Leo upo kazini lakini kesho unaweza usiwepo kazini. Leo unasoma kesho utamaliza shule, lakini utakosa ajira. Badili namna ya kufikiri. Anza kufikiri endapo hutakuwa na kazi maisha yatakuwaje? Na kama unasoma ukakosa ajira itakuwaje. Leo una nguvu kesho zitapungua. Uwezo wa kufikiri nao utapungua.

Ni vyema ukatumia muda huu kufanya mambo yenye tija, ambayo pia yatasababisha fikra za wengine kubadilika.

Mungu akubariki kwa kuisoma makala hii, naamini kuwa utabadili namna ya kufikiri. Kama ulikuwa ukifikiri kwa kiwango cha chini sasa utaanza kufikiri kwa kiwango cha juu kabisa.
Fikra zako zitasababisha uweze kufika pale unapotaka.
Huna sababu ya kuishia njiani
Bali una kila sababu ya kuhakikisha unafikia Ushindi mkubwa.

Ahsante sana

Ni mimi rafiki yako.
Steven Mshiu
+255 655 882074
+255 768 882074
smshiu42@gmail.com

Alhamisi, 27 Julai 2017

JIFUNZE KWA NDEGE WA ANGANI

JIFUNZE KUTOKA KWA NDEGE WA ANGANI.
Image may contain: 2 people, people smiling, people standing Na Steven Mshiu
Ndege ni miongoni mwa viumbe hai aliowaumba Mungu. Na alipowaumba aliwaweka chini ya utawala wa mwanadamu. Maisha ya ndege ni ya uhuru sana. Yupo tayari kwenda popote pale anapopataka tena kwa wakati.
Mungu alipowaumba alifafahamu kuwa watakula wapi na watalala wapi. Mahali pengine Yesu mwenyewe akasema tusisumbukie maisha yetu, tuwaangalie ndege wa angani. Wao hawana shamba lakini Mungu huwalisha. Sasa kwetu sisi wanadamu si zaidi ya hao ndege?

Maisha ya ndege hutegemea kiota kama sehemu ya kulala, kuishi na kuzaliana. Kiota hicho mara nyingi ndege hukijenga kwenye tawi linaloningi'inia. Hutumia muda mrefu kukijenga kiota hicho. Tulipokuwa watoto tulikuwa tukiviharibu viota hivyo, lakini cha ajabu ndege yule huangalia tawi lingine na kuanza kujenga kiota kingine kipya.
Kiota kile hukitumia kwa muda hasa pale anapojiandaa kutaga, na baada ya kumaliza kutaga huyaatamia yale mayai hatimaye hutotoa makinda ya ndege.

Hutumia juhudi nyingi kuhakikisha yale makinda yanakuwa ndege kamili, na baada ya hapo huhama kwenye kiota kile na kusonga mbele kwa mbele. Maisha yanaendelea kama kawaida.
Kitu nilichotaka tujifunze kupitia ndege ni kwamba yeye anategemea ule uwezo aliopewa na Mungu, Jana nilikuwa nakatiza maeneo fulani nikakutana na kundi kubwa sana la ndege. Walikuwa wamekusanyika kwenye mti uliokuwa na matawi mengi sana, Kwa kuwa ilikuwa ni majira ya jioni hivyo upepo ulikuwa ukivuma,

Niliyaona matawi yakienda huku na kule, yaani yakienda jinsi upepo ulivyokuwa ukivuma. Lakini jambo la kushangaza sikuwaona wale ndege wakihofia matawi labda kutokana na upepo kuwa mkali, tawi linaweza kuvunjika hivyo likahatarisha maisha yao.

Nilipoendelea kuwaza zaidi ndipo nikakumbuka kuwa ndege hawategemei sana yale matawi ya ule mti. tegemeo kubwa la ndege lipo kwenye mbawa zake. Kama tawi likivunjika wakati wowote, basi wataruka kwa kutumia msaada wa mbawa zao na kutafuta tawi lingine.

MAMBO YA KUJIFUNZA
Kuna watu Mungu amewapa vitu vizuri sana ikiwa ni pamoja na akili lakini hawajui ni kwanini au ni kwa sababu gani wamepewa.
Mara nyingi katika maisha yrtu kuna mambo au changamoto tunakutana nazo zinatufanya tuondoe lengo kwa Mungu na kuliweka sehemu fulani. Unaweza kuwa unasoma mchakato wa ada ukawa ni mgumu ukaweka tumaini lako kwa ndugu yako maana ana uwezo kidogo. Nataka nikukumbushe kuwa huyo ndugu ni kama tawi. Kuna siku upepo utavuma halafu litavunjika. Jiulize kama ndio umeshika kwenye tawi hilo matokeo yake yatakuwaje?

Kuna watu Mungu amewabariki kwa vitu vichache tu. Wakasahau kuwa ni Mungu kawawezesha kuvipata. Imani yao wakaiweka kwenye vitu hivyo. Hawana tena hata muda wa kumfanyia Mungu ibada. Mtu yuko bize jumatatu hadi jumatatu. Nakukumbusha kuwa vitu hivyo ni kama tawi tu. Siku upepo ukivuma kwa kasi yawezekana tawi hilo likavunjika. Upepo naufananisha na majaribu. Mpendwa hali yako itakuwa ni mbaya zaidi.

Kuna watu wana nia ya kufanya mambo makubwa kwa ajili ya kutimiza kusudi Mungu alilowaumbia. Lakini hali ya kukatishwa tamaa na kurudishwa nyuma inapowakabilli basi basi huona ni bora kuishia njiani kabisa. Hukata tamaa na kurudi nyuma. Tulipoharibu viota vya wale ndege, kesho yake tulikuta wamejenga kiota kipya tayari.

Maisha yanahitaji watu jasiri. Watu wasiokata tamaa. Watu wasiochoka kujaribu kufanya kitu kipya. Mungu naye anamhitaji mtu asiyeangalia nyuma. Kuangalia nyuma ni ishara ya kushindwa, Muulize mke wa Lutu kilichomkuta kisa kuangalia nyuma. Askari anaeangalia nyuma au kurud nyuma hupigwa risasi na kikosi kinachobakia husonga mbele kwa ajili ya kuutafuta ushindi.

Jaribu kufanya kitu kipya leo.

Ishi maisha yenye UHURU. Nikisema maisha yenye uhuru simaanishi ufanye unavyotaka. Ndege wana uhuru wa kutosha. Hakuna kiumbe kinachowapigia kengele kuwa muda wa kuamka umefika. Hakuna kiumbe kinachowaambia kuwa ni muda wa kwenda kutafuta chakula, au ni muda wa kurudi kwenye kiota chake. Wao wamejipangia ratiba zao vizuri. Uhuru unatokana na kujijengea nidhamu binafsi.

Kuna watu wanapokuwa karibu na wazazi wao huishi maisha fulani na wanapotoka karibu na wazazi wao huishi maisha tofauti kabisa. Yaani mtu ana wokovu wa nyumbani tu, Akitoka nyumbani hana wokovu. Biblia inasema katika Yohana 8; 33 na kuendelea kuwa mtu anapoifahamu KWELI huwa HURU kwelikweli.
Jifunze kujitegemea. Mungu hakumuumba mtu ili awe tegemezi. Utegemezi huanza pale mtu anapojisahau na kutoka kwenye lengo lake yaani kusudi. Ndege wao hawamtegemei mtu. Tegemeo lao kubwa lipo kwa aliewaumba tu. Pale unapoonyesha juhudi zako kuwa unaweza ndipo Mungu naye hukuwezesha. Epuka kumtegemea mtu au kitu, maana wakat wowote vitu vyaweza toweka. watu nao waweza toweka.

Jambo la mwisho kumbuka kuwa Mungu amekupa uwezo wa kuhimili kila aina ya kimbunga au upepo unaovuma katika maisha yako. Hakuna mwanadamu ambaye anaweza kuyakwepa majaribu. Imani yetu ni kama mbawa za ndege. Pale kimbunga cha majaribu kinapotaka kutuzamisha basi kupitia mbawa za imani yetu tunaweza kuruka juu zaidi na tukafikia ushindi mkubwa sana.
Mpendwa rafiki,

Natamani niendelee kuandika zaidi na zaidi lakini kwa machache haya ni imani yangu kuwa kuna jambo moja au mawili utakuwa umejifunza.

Nakutia moyo kuwa huna sababu hata moja ya kuishia njiani ila una sababu nyingi tu za kuinuka na kusonga mbele na hatimaye ukaweza kufikia USHINDI MKUBWA SANA.
Mungu akubariki sana kama utasoma waraka huu hadi mwisho na ukiupenda waweza mshirikisha na mwenzio.

Rafiki yako.
Steven Mshiu
+255 655 882074
+255 768 882074
smshiu42@gmail.com

Jumatano, 26 Julai 2017

THAMANI YAKO NI KUBWA SANA.

THAMANI YAKO NI ZAIDI YA CHOCHOTE.
Na Steven Mshiu.
Sikupenda siku ya leo ipite hivi hivi bila kukukumbusha angalau kitu kimoja.
Siku mbili zilizopita nilikuwa nina shida na mtu fulani, na nisingeweza kumpata pasipo kutumia mawasiliano ya simu. Kwa bahati nzuri nina simu ya mkononi. Kilichofuata niliamua kununua vocha yenye thamani ya shs. 5,000/-
Kwa kuwa mtu niliyetaka kuwasiliana naye alikuwa yupo nje nje ya nchi ilinibidi niihifadhi ile vocha kwa umakini mkubwa saaana, niliitunza sana kwa muda wa masaa saba hivi, akili yangu yote ilikuwa ikiiwaza ile vocha. Kwamba muda utafika saa ngapi ili niitumie,
Ilipofika majira ya saa nne na nusu hivi nyakati za usiku tayari giza lilikuwa limeshaifunika dunia, niliitoa ile vocha na kuwasha tochi ya simu yangu hatimaye nikaibadilisha ile vocha kuwa muda wa maongezi.
Baada ya kuiingiza ile vocha kwenye simu yangu kabla sijazima tochi ya simu tayari kile kikadi cha vocha chenye thamani ya 5000 nilishakitupa chini na kukisahau, kwani ile thamani yake ilishahamia kwenye simu yangu.
Cha ajabu sikuwa na muda wa kuiwazia tena ile kadi. HAtimaye nikafanya mawasiliano na yule ndugu niliyekusudia na mambo mengine yakaendelea.
Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Roho Mtakatifu akaanza kunifundisha vitu vyake.
Nikajifunza kuwa maisha yetu yana thamani kubwa sana, ni zaidi ya thamani ya madini ya aina yoyote ile.
Akanifundisha kuwa miili yetu huwa na thamani kabla haijatumika vibaya. Ikishatumika vibaya ule ubora wake hupotea kabisa,
Sasa basi acha leo niwakumbushe vijana wenzangu hususani mabinti. Nimekuwa nikisikia kuwa kuna mabinti ambao wamefanya miili yao kama chanzo cha mafanikio. Kuna ambao wako vyuoni lakini ili wafaulu wanaamua kuitoa miili yao kwa walimu ili wasifeli. Wengine ili wapate kazi wanadiriki kulala na waajiri wao ilhali wapate ajira tu.
Yaani hawaamini kama Mungu anaweza kuwapa kile wanachohitaji pasipo kutoa rushwa ya miili yao.
Leo nataka nikukumbushe jambo hili. Hao unaojirahisisha kwao wamekufanya Kuwa kama VOCHA. Wanakuthamini kabla hawajakutumia. Ile haja ya nafsi zao yenye uovu ikishatimia wanakutupa kama mimi nilivyotupa ile kadi ya VOCHA niliyokwisha kuitumia,
Wakishakutumia watakutupa. Tena watakutupa gizani. Tena wakiwa wamezima taa. Hawatakujali tena. Huyo lecturer akishamaliza haja yake atatafuta mwingine tena. Hata mimi baada ya kuitumia ile vocha ilipokwisha nilienda kutafuta nyingine siku iliyofuata. Huyo kijana unaeenda kujirahisisha kwake, eti ni wachumba unakaa kwake, sijui unamfulia eti kakuambia atakuoa, mwishowe anakuingiza chumbani na kutekeleza azma yake aisee ukishafanya hivyo ndio imekula kwako.
Tayari hapo ni VOCHA imeshatumika mzee, Jiandae kisaikolojia kutupwa na kukanyagwa na watu wengine. Na usitegemee tena ile thamani yako kurudi.
Vijana wenzangu tujiheshimu. Tusikubali mtu yeyote atutumie kama anavyopenda yeye. Tunahitaji kuitunza thamani yetu.
Mara nyingi huwa napenda kusema kauli hii kuwa JIHESHIMU ILI UHESHIMIWE. Hakuna mtu atakayekuheshimu ilhali wewe umeshaji-devaluate.
Ukitaka watu wakusifu ni pale unapoonyesha msimamo wako na uthamani wako.
Leo una nafasi ya kumwonyesha huyo lecturer kuwa wewe ni wa thamani ipi,
Una nafasi ya kumwonyesha huyo Bosi kuwa wewe ni wa thmani ipi.
Una nafasi ya kumwonyesha huyo kijana anayekudanganya kuwa wewe sio wa bei rahisi.
Una nafasi ya kuonyesha uthamani wako.
Zile sifa zitakazotoka kwa watu, kama anavyosifiwa binti aliyeitunza thamani yake katika Mithali 31:29, utazisikia kwa wengine tu. Wale waliokataa kuipoteza thamani yao.
Nikutie moyo ewe binti, Ingawa unakutana na changamoto hizi nyingi, Usijaribu kutumika kama VOCHA. Itunze thamani yako. Jiamini kuwa unaweza bila hata kuutumia mwili wako kama chanzo, cha kupata mafanikio. Mungu amekupa akili na uwezo. Itumie akili na uwezo vyema hakika utafanikiwa.
Ondoa ile dhana kuwa ukiutoa mwili wako bwererer bwerere ndio utapata mafanikio ya haraka kwa kirahisi. Aliwahi nifundisha mtu mmoja kuwa siku zote RAHISI NI GHALI ZAIDI. Kile kitu unachokipata kwa urahisi kwa kutumia njia rahisi rahisi huwa kinagharimu sana.
Nataka leo uchukue hatua. Hatua ya kumwonyesha kila mtu thamani yako.
Baada ya muda mchache utakuja kunipa ushuhuda wa ushindi mkubwa sana wenye matokeo chanya.
Kama ujumbe huu utakugusa natoa ruhusa ya kuu-share popote pale ili tuwakumbushe wengine kuitunza thamani yao.
Ubarikiwe sana.
Rafiki yako,
Steven Mshiu.
+255 655 882074
+255 768 882074,

MAMBO YA MSINGI KWA KIJANA

MAMBO SITA YA MSINGI ANAYOTAKIWA NAYO KIJANA ILI AWEZE KUKUBALIKA KATIKA JAMII.
Na, Steven Mshiu.
Leo ninawiwa kukuletea makala hii, "MAMBO 6 YA MSINGI ANAYOTAKIWA KUWA NAYO KIJANA ILI AKUBALIKE KATIKA JAMII". Lakini acha nianze kwa kusema hivi, binafsi nina hofu kubwa sana kwa "taifa la kesho" ambalo asilimia kubwa ni sisi vijana maana tumekosa muelekeo, na kupoteza uthamani wetu.
Taifa linategemea vijana, familia kama familia inategemea vijana, makampuni mengi yanategemea vijana, hata kanisa nalo linategemea vijana, kwanini? Kwa sababu vijana tuna nguvu, yani ni tofauti na watu wa umri mwingne kama wazee na watoto. Hata biblia inasema hivyo. Lakini cha ajabu tumeshindwa kujitambua kuwa sisi ni akina nani na tunapaswa kufanya nini. Ole wetu vijana.
Kutokana na hali hii jamii imeshindwa kutupa kipaumbele kwa ajili ya kukosa mambo haya sita ambayo tutayaangalia japo kwa kifupi kutoka 1 Thimotheo 4:11-12, Mwandishi wa maneno haya alikuwa ni Paulo aliyejulikana kwa jina la Sauli ambaye alikuwa na kazi ya kuwaua watumishi wa Mungu waliokuwa wakiifundisha KWELI ya MUNGU. Na alikuwa akimwandikia mwanae katika huduma aliyejulikana kwa jina la Timotheo.
Ingawa Timotheo alikuwa ni mdogo kiumri, lakini Paulo alitaka kumthibitishia kuwa atakapotambua kile kilichopo ndani yake yaani kusudi lake hakika jamii itamheshimu na pia itaheshimu ile huduma yake. Mwandishi anasema mtu yeyote asiudharau ujana wako bali uwe.
1. Kielelezo.
Kuwa kielelezo ina maana ni kuwa mfano, kitu cha kuigwa. Watu wa"copy" kutoka kwako. Sasa tumekuwa hatuna cha kuigwa katika jamii, badala yake ndo walevi "wanywa viroba" kuwa na tabia zisizo njema kama wizi, uporaji n.k.
Ukija kwenye suala la uvaaji ndio hatari kabisa, dada zetu wanavaa nguo zinazonesha miili yao"transparency" vijana wa kiume nao suruali chini ya makalio,. Yani jamii inashindwa kutuelewa kabisa. Vijana wengi wa siku za leo hatuna kitu chochote ambacho jamii itaiga kwetu. Hii ni hatari kubwa sana. Hebu tubadilike.
2. Usemi.
Kauli/usemi ndiyo inayomfanya mtu kukubalika mahali popote pale. Watu wanakutambua kwa jinsi unavyoongea tu. Kwa utafiti mdogo nilioufanya nimegundua kuwa vijana ndio wenye majibu ya "hovyo" mahali popote pale. Ukikuta binti anajibizana na mama yake huwezi amini kama anamjibu mzazi wake hvyo.
Sasa kupitia kauli zetu na jinsi tunavyo"communicate"¬ na watu kumetufanya tukawa tunakosa fursa mbalimbali na hata kushirikishwa kwenye jambo lolote lile linalohitaji maamuzi au mchango wa kijana. Hali hii inatufanya tunakosa haki zetu za msingi.
3. Mwenendo
Jamii inatazamia kuwa mwenendo wa kijana unatakiwa kuwa mzuri, lakini badala yake, inatuona tunaenenda katika njia zisizofaa kama ukahaba, ulevi, wizi na kujiunga na vikundi vya uhalifu n,k, jamii inatudharau. Kumbuka nilianza kwa kusema kuwa "mtu yoyote asiudharau ujana wako" lakni hapa sisi tunakuwa chanzo cha kudharaulika. Hebu tubadilishe mwenendo wetu kuwa mzuri.
4. Upendo.
Kama kijana utakosa kuwa na upendo kwa jamii inayokuzunguka, itakuwa ni ngumu sana kupata msaada. Jamii itakutelekeza. Ukitaka jamii yako ikupende, ipende wewe kwanza. Kila mtu atatamani kuuona uwepo wako. Fursa nyingi zitakua zinakuangukia wewe maana una mahusiano mazuri na jamii yako.
5. Imani.
Hili ni jambo lingne la muhimu sana kwa maisha ya kimwili na kiroho. Ili umpendeze Mungu ni lazima kuwa na imani. Biblia inasema kuwa "Hauwezi kumpendeza Mungu kama huna imani". Jamii inapenda mtu anaemwamini Mungu, maana hata yeye mwenyewe ataaminika. Siku hizi ofisi nyingi zinaogopa kuwaajiri vijana, kwa sababu hazina imani na sisi. Tunakosa mambo mengi kwa sababu hatuamiki. Tubadilike. Tukitaka kula "mema ya nchi" hebu tujiaminishe kwa jamii. Tusiwe watu wa kutiliwa mashaka kila mahali.
6. Usafi.
Hapa sizungumzii usafi wa kimwili tu. Maana mwili huu ni kama "mother body" ya roho zetu. Japo ni lazima uuweke katika hali nzuri. Hata biblia inasema itunzeni miili yenu maana ni hekalu la roho mtakatifu. Utakapoamua kuwa msafi kiroho, yaani kuacha mambo yote mabaya i.e dhambi, hata kimwili utakuwa safi pia. Mabadiliko huanzia ndani na matokeo ndio yanayoonekana kwa nje. Mungu anapenda usafi. Mara nyingi alipotaka kukutana na wanadamu kama ni msomi wa Biblia kile kipindi cha Musa, alimwambia awaambie wana wa Israel wafue mavazi yao.
Hapa hakumaanisha mavazi ya kawaida. Alikuwa anasisitiza Usafi wa moyo yaani utakatifu. Kitu kisafi ni kitu kisichokuwa na doa lolote. Dhambi ni doa. Kumbuka dhambi ndiyo iliyomtenga mwanadamu na Mungu. Lakini kwa ajili ya usafi na Utakatifu wa Mungu alimtoa Yesu ili kuyafuta yale madoa yetu.
Mahali pengine anatulazimisha kuwa watakatifu. kwa kuwa yeye mwenyewe ni mtakatifu. Siku moja niliwahi kuwaambia watu fulani kuwa matokeo ya hali zetu za sasa ni madhihirisho ya hali za viroho vyetu. Kwamba kila kinachotokea physically tayari kilishatokea katika roho. Viroho vyetu vikiwa visafi hata muonekano wetu wa nje unakuwa nadhifu.
Hatua za kuchukua kwa haraka:
Kwanza ni lazima kijana ajitambue yeye ni nani na yupo kwa kusudi gani. Kujitambua ni hatua ya kwanza kabisa.
Pili, Aelewe jamii inayomzunguka inamhitaji. Inahitaji Nguvu zake. Inahitaji mchango wake. Kijana akishafahamu uhitaji wa jamii inayomzunguka, haitakuwa ngumu kwake kupata fursa.
Tatu, Bado una nafasi ya kurekebisha pale ulipoharibu. Mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa kuanguka sio tatizo. Tatizo ni pale unapoendelea kubakia pale chini.
Nne, Kijana awe na maono pamoja na malengo madhubuti.
Naamini utakuwa umejifunza mengi, na ninategemea mabadiliko makubwa sana. Nimalizie kwa msemo huu, "CHANGES IN OUR SOCIETIES DEPENDS THE CHANGES OF YOUTHS FIRST".
Nimependa kuirudia makala hii. Niliiandika miaka kadhaa iliyopita. Lakini nimeona kuna haja ya kuwakumbusha tena vijana wenzangu mambo haya.
Hakika tunahitaji kubadilisha mitazamo yetu ikiwa ni pamoja na mfumo wa maisha tunayoyaishi
Imeandikwa na,
Steven Mshiu
+255 655 882074
+255 768 882074
Barua pepe; smshiu42@gmail.comwww.inukauangaze.com

USIJIDHARAU

#USIISHIE_NJIANI
USIJIDHARAU.

Na Steven Mshiu.
Nina kila sababu ya kumtukuza na kumuinua Mungu wa mbinguni kwa kunipa nguvu na afya tele. Mungu ametupa wiki nzuri ambayo ni ya ushindi mkubwa kwako wewe uliyedhamiria kuupata. Jambo la msingi ni kuweka juhudi kubwa juu ya kile unachokifanya ambacho kina matokeo chanya. Mara nyingi huwa napenda kusema kitu chenye matokeo chanya maana unaweza jikuta unafanya vitu ambavyo havifai na havina utukufu.

Siku moja nilikuwa katika kusanyiko Fulani. Kwa bahati nzuri tulikuwa ni vijana. Mimi nikiwa kama msemaji mkuu wa kusanyiko hilo nilim-appoint mmoja miongoni mwa vijana wale kutuongoza katika pambio la kuabudu. Kimuonekano niliamini anaweza kufanya hivyo, maana kama ni sauti anayo tena nzuri tu,

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida huku vijana wote tukiwa tumesimama na kufumba macho, ukimya wa zaidi ya sekunde 45 ulitawala bila kumsikia Yule kijana niliemteua atupatie pambio ya kuabudu akianzisha wimbo. Basi nikaamua kuimba mimi mwenyewe kuliko kuendelea kupoteza muda.

Baada ya mambo yote nikamuita Yule kijana na kumhoji mambo kadhaa. Nikamuuliza kwanini hakuimba pambio? Nini kimemsibu? Je alikuwa ni mgonjwa?

Kati ya maswali yote niliyomuuliza majibu yake yalikuwa ni “HAKUNA”. Akaniambia kuwa yeye hawezi kabisa kuimba. Nikamuuliza unaweza kufanya nini sasa. Je kuomba? Looh!! Akawa mkali kabisa akasema hapo ndio hawezi kabisaaa..

Anyway. Nikawa nimejifunza mambo mengi sana. Kupitia kijana huyu. Unajua kuwa Mungu amewaumba wanadamu wote sawa. Hakuna aliyempendelea hata mmoja. Wala hakuna aliyeumbiwa kushindwa jambo lolote. Ila mwanadamu huyu kwa kushindwa kulitambua kusudi lake au kujitambua mwenyewe akaamua kujitengenezea mazingira ya kushindwa yeye peke yake.

Nilikuwa nasikiliza Audio moja ya kijana mmoja amabaye ni mwandishi na mhamasishaji kwenye group la WhatsApp akawa anafafanua kuwa akili ya mtu inapokea yale maneno anayoyazungunza na kuanza kuyafanyia kazi kwa haraka sana. Yaani kwa mfano ukisema huwezi instant akili yako inachukua lile neno siwezi na kuanza kulifanyia kazi, na huwa inaleta matokeo sahihi ambayo ni SIWEZI.

Tuko hapa tulipo kutokana na mazingira ambayo tumejijengea. Upo hapo ulipo au jinsi ulivyo kulingana na kile ulichoamua akili yako ikifanyie kazi.

Kipindi Fulani Mungu alimtaka Gideoni akapambane na Wamidian, Taifa lililowatesa Israel kwa kipindi kirefu sana. Gideoni akaanza kuwaza how comes yeye ataenda kupambana na hao wamidiani. Akairuhusu akili yake iwaone Wamidiani kuwa ni tatizo na hana namna ya kuweza kupambana nao. Akili yake ikamletea majibu mazuri tu. KUmbuka akili yako ni kama kiwanda. Akili ya Gideoni ikazalisha “bidhaa” ya woga. Ikamuelekeza akajifiche mapangoni.

Kumbuka kusudi la Mungu kwa Gideoni ni kuwa Mungu anamuona yeye kuwa ni shujaa. Mungu anaamua kumfuata Gideon kule kule mapangoni na kumtia moyo kuwa yeye ni shujaa na atawaokoa Israel dhidi ya Wamidian.

Kwa sababu akili ya Gideon ilishaathirika Mungu anaamua kufanya kazi ya ziada kumtia moyo Gideon, Mungu anamwambia aende kwa ule uwezo wake naye Mungu atajidhihirisha kwake. Lakini Gideon hakuridhika na majibu ya Mungu akawa anataka uthibitisho wa kutosha kutoka kwake, naye Mungu hakusita kufanya hivyo.

Baada ya moyo na akili ya Gideon kupona, ile sumu ya kujiona hawezi imeshaondoka, Gideon anaandaa jeshi la watu elfu 32, ili kwenda kupambana na jeshi la Wamidian lenye wanajeshi zaidi ya laki na thelathini. Kwa akili za kawaida ni ngumu kuamini, yaani mwanajeshi mmoja wa kikosi cha Gideon akapambane na wanajeshi wane wa Wamidian.

Kwa sababu Gideon ameshajivika hali ya ushujaa na kujiona Kuwa ni mshindi Mungu anamwambia hao wanajeshi ni wengi, hivyo awapunguze, Hatimaye wakapungua hadi kufikia idadi ya wanajeshi mia tatu tu (kumbuka hawa wanajeshi mia tatu wanaenda kupambana na wanajeshi laki na thelathini)
Nataka nikuonyeshe kitu kimoja hapa, Ukibaki ukiwa unajiangalia hali yako, unaangalia mazingira yako, unalinganisha na ukubwa wa tatizo lako, akili yako itakuletea kushindwa tu. Gideon akaamua kwenda na kundi lile la wanajeshi mia tatu lililogawanyika kwenye vikundi vitatu vya wanajeshi mia moja kila kikundi. Kwa hesabu ya haraka ni sawa na mwanajeshi mmoja wa Gideon anapambana na wanajeshi 440 wa Wamidian.

Nataka nikuambie kuwa huwezi kuamini Gideoni aliwapiga Wamidian kama vile panzi. Gideon wakapata ushindi mkubwa sana. Mungu akajithibitisha kwa viwango vya ajabu. Unajua ni kwanini? Gideon na jeshi lake waliweka kando ile dhana ya kushindwa na kukikiri kile Mungu alichowaambia Kwamba wao ni MASHUJAA (Ukipata muda soma Waamuzi sura ya sita nay a saba)

Watu Fulani kwenye Biblia wakaenda kuipeleleza nchi ya Kanaani wakarudi na majibu ya kukatisha tama kabisa. Wakasema kuwa nchi ile ni nzuri sana na ina kila kitu lakini watu wanaokaa katika nchi hiyo ni majitu, yaani wanawala watu wakaao katika nchi hiyo. Wakajiona wao ni kama panzi tuu. Lakini anatokea Joshua na Kalebu wanawatia watu moyo kuwa wanaweza kuimiliki nchi ile.

Nataka nikukumbushe kuwa Mungu hayuko radhi na mtu anaejidharau. Kitendo cha mwanadamu kujidhararau ni kumdharau Mungu. Tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Pumzi yetu tumepewa na Mungu hii inamaanisha kuwa Mungu anaishi ndani yetu. Hivyo ukijidharau tu aisee jiandae kupigwa na Mungu
Mara nyingi tumekuwa tukisoma maamndiko kuwa hakuna jambo ambalo linamshinda Mungu,. Usifikiri Mungu atashuka mwenyewe aje afanye jambo. Kama akishuka yeye hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kuhimili. Badala yake Mungu anamtumia mtu kufanya jambo. Alimtumia Gideon kuwapiga Wamidian. Alimtumia Daudi kumuua Goliath. Usifikiri zilikuwa ni nguvu za Samson peke yake kuweza kuwapiga watu laki na themanini kwa taya la punda. Hapana. Ni Mungu alikuwa anafanya kazi kupitia Samson.

NAtamani uondoke kwenye hiyo hali ya SIWEZI. Nataka ujione ukiwa shujaa kama Gideon. Unapojidharau ukajiona huwezi kumbuka kuwa hata watu wengine wanaathirika sana. Taifa la Israel lilifadhaika sana kutokana na majibu waliyoletewa na wale wazee 12 waliokwenda kuipeleleza nchi ya Kanaani
INUKA
Anza safari mpya leo. Anza kufanya kile ulichosema huwezi kukifanya. Anza kufanya kile ulichoshindwa. Niliwahi kusema kuwa kile unachoogopa kukifanya ndicho kilichobeba mafanikio yako. Kikwazo chako ndio mafanikio yako. Huna haja ya kuishia njiani, Nikthibitishie utakapoanza mwanzo mpya hakika utafikia ushindi mkubwa sana
Kama utabarikiwa na ujumbe huu ni ruksa kushea popote ili unisaidie kumkumbusha mtu mmoja kuwa asijidharau, ana nafasi ya kufikia ushindi mkubwa hivyo asiishie njiani.
Ahsante na ubarikiwe sana.

Ni mimi rafiki yako
Steven Mshiu
+255 768 882074
+255 655 882074
Smshiu42@gmail.com

MAKUNDI MAWILI YA WATU WANAOKUZUNGUKA.

FAHAMU MAKUNDI MAWILI YA WATU KATIKA MAISHA YAKO. Na Steven Mshiu . Maisha ya kila mwanadamu yamezungukwa na watu. Watu hawa waweza kat...